mbadala wa ndoa


great thinking hii mkuu, big up
 
great thinking hii mkuu, big up

umejaribu kufafanua vya kutosha, mkuu. Nilisoma post ya mdau mmoja hapa na wazo kama hilo la kubadili mfumo mzima likanijia na hapo nikachoka. Tatizo ni kuonana kila muda na kuzoeana
 


umejaribu kufafanua vya kutosha, mkuu. Nilisoma post ya mdau mmoja hapa na wazo kama hilo la kubadili mfumo mzima likanijia na hapo nikachoka. Tatizo ni kuonana kila muda na kuzoeana
 
Kitu tunachokisahau kabla ya kufunga ndoa,unapokuwa kwenye mapenzi makali,unafikiri kila kitu kinawezekana. Unasahau kuna siku urafiki huu utakwisha...utachoka na tabia ya huyu mwenzako uliyoivumilia ili mwe pamoja (kwa kipindi cha mapenzi makali)....utasahau kwamba mlikutana ukubwani na hamkulelewa na mama mmoja....na vitu vingi kibao ambavyo watu wengi hawavifikirii kabla. tunadhani mtu anaweza kubadilika....how? kama alikuwa akibadilisha wanawake/wanaume kama nguo,wewe ni nani wa kumfanya atulie? hatujiulizi maswali lukuki yanayoweza kutufanya kamwe tusiingie kwenye huu mkataba wa milele.
Uvumilivu unaotakiwa kwenye ndoa una-cost maisha,afya na rasilimali ulizonazo. na je watu wanapendana kweli au wanatamaniana tu? wanaposema I DO! inatoka moyoni au wanaogopa umati unaowatazama?
Wenzetu wa Magharibi baada ya kuona matatizo haya,waliamua kuihamishia ndoa kwenye mkataba. Unasaini kwa kipindi fulani halafu mkiona kuna haja ya kuongeza muda then mnaongeza. Mkichokana/ukichoka unaondoka kabla ya ngumi na maneno.
Nafikiri ungekuwepo mbadala hasa kwa wanawake kwa kiafrika nafikiri wengo wangekuwa na tabasamu midomoni mwao,maisha marefu ya furaha!
 
niliwaza sana haya zamani lakini kuna kipindi kinakuja chenyewe pale unapohitaji msaidizi katika maisha

Msaidizi wa nini? Maana sijasema usiwe na uhusiano. Nachosema ni kutokuoa ama kuolewa. Unaweza kabisa ukawa na uhusiano na mwenzako bila kuoana na mka define terms za uhusiano wenu. Ila mkishaingia kwenye ndoa kunakuwa na matarajio kibao ambayo mengine wala si realistic na ndio inakuwa mwanzo wa misery.
 
Kwa mawazo yenu wadau ningependa kuona ni jhnsi gani mtu anaepuka misery na kuwa furahani wakati wote kama katika kipindi cha uchumba. Tukiongelea mikataba itabidi mfumo wa maisha uwe tofauti na huu wa sasa kwa maana mikataba yaweza ponya upande mmoja na kuanzisha gonjwa upande mwingine
 
Kwa mawazo yenu wadau ningependa kuona ni jhnsi gani mtu anaepuka misery na kuwa furahani wakati wote kama katika kipindi cha uchumba.

Sio rahisi sana uhusiano ukabaki kama ilivyokuwa kipindi cha uchumba. Kipindi cha uchumba kina malengo tofauti na yale ya baada ya kuoana (naweza kufanya analogy ya kipindi cha uchumba na kipindi cha kampeni katika siasa!).

Kwa ajili ya mjadala huu naweza kugawa maisha ya ndoa katika hatua tau/vipindi vitatu:

Hatua ya kwanza (tuiite 'pretence and learning'): Inaanzia kwenye uchumba mpaka say mwaka mmoja au miwili baada ya ndoa. Hapa uhusiano unakuwa mzuri sana kwa sababu kila mmoja anajaribu kumpendeza mwenzake na kumuonesha kuwa yeye ni chaguo bora/sahihi (hii kwa walio wengi inaambatana na uongo/pretence kwa wingi sana). Kuna maelewando na kusameheana. Baadhi ya kasoro au mapungufu 'yanafichwa' au 'yanavumiliwa'. Hapa ndo utaona maua, kadi na vitu kama hivyo baina ya wapenzi.

Lakini kadri stage hii inavyoendelea wanandoa wanaanza kuonesha 'rangi' zao halisi na/au kuona 'rangi' halisi ya mwenza wake. Kwa kujibu swali lako, ni vema katika stage hii ukapunguza pretence na kuweka wazi vitu unavyoona ni kasoro/mapungufu kwa kadri uwezavyo (kumbuka sio rahisi kuiepuka pretence kwa 100%).

Hatua ya pili (hii tuiite 'reality'): Hapa wanandoa wameshafahamiana (mazuri na mabaya) na wanatoka kwenye pretence na kuingia kwenye reality (a spade will be called a spade!). Kila mmoja anabehave kiuhalisia kabisa (anaonesha 'rangi' yake bila woga). Sasa level hii huchukuwa muda mrefu sana na ndio kipindi cha matatizo mengi ya ndoa hasa hasa kama kuna vitu vingi 'vilifichwa' au 'havikuonekana' katika level ya kwanza.

Hatua ya tatu (hii tuiite 'maturity'): Katika kipindi hiki tayari wanandoa wameshapitia mikimiki yote ya hatua ya pili. 'Majeraha' mengi tayari 'yamepona'! Hiki ni kipindi kitamu na cha shukrani. Unasema "bila mama/baba nanii, nisingekuwa hapa". Laikini hili litategemea jinsi mlivyoweza kushughulikia matatizo katika hatua yenu ya pili. kumbuka 'majeraha' mengine yanaweza kusababisha 'ulemavu' hivyo bado kukawa na kinyongo na kulaumiana. Uzuri wa kipindi hiki wanandoa wanakuwa wameshakubali hali halisi whether ni mbaya au nzuri na wanaweza kuvumilia.

Binafsi nipo hatua ya pili na mambo sio rahisi hivyo lakini namshukuru mungu ndoa yangu bado imesimama🙂!
 

big up kwa maono hayo. kwa maoni haya na mengine, ndoa inakuwa kama kipande/sehemu ya mwili wa mtu. mfano rangi, nywele, sura, au umbo. sasa kama hupendi kimojawapo kati ya hivyo kwenye mwili wako huna jinsi ya kukiepuka zaidi ya kukubali tu hali halisi. ndoa ni mpango/mfumo wa maisha ambao inaonekana hauwezi kuepukwa pamoja na mapungufu yake. binafsi nisingependa maishani nije kujutia kwa nini nilioa. kwa upande mwingine ni vigumu kuishi bila ya mwenza kwa namna Mungu alivyotuumba. katika kuhakikisha kuwa tunakabili mihamko yetu, tunakuwa na wenza ambao inafuata taratibu kuwa nao. kwa inavyoonekana, bila kufuata utaratibu itakuwa ni balaa katika tasnia nzima ya mahusiano. kwa vile ndoa ni mpango wa Mungu basi hauna mbadala? na inavyoonekana huu mfumo wa sasa unajaribu tu kupunguza maafa ambayo yangesababishwa na kutokuwepo kwa ndoa japo ndoa nayo ni sehemu ya matatizo. the best solution hapa ni kuwa na uvumilivu
 


MUME SIO BABA YAKO AKUNG'ANG'ANIE AU MKE SIO MAMA YAKO AKUNG'ANG'ANIE Pls listen to your heart, days are numbered
 
niliwaza sana haya zamani lakini kuna kipindi kinakuja chenyewe pale unapohitaji msaidizi katika maisha


Eti, FL akusaidie nini????? Money?, pleasure? sex? company or what?? better to stay single if you want to get rid of marriage calamities
 

Duuuuuuu! Mgombe Ubunge labda uko kwenye kampeni za ubunge zaidi kuliko thread yenyewe inavyosema. Ugomvi ndani ya ndoa unatokana na sababu za msingi. Hizo ulizozisema ni chembe tu ya sababu halisi. Waliopo kwenye ndoa mtasaidia hapa. Mapenzi sio fedha, mali mliyonayo wanandoa. Mapenzi ni mapenzi kati yenu ninyi wawili tu hakuna tarishi mtakayemwajiri awe ndio muuaarobaini wa matatizo ya ndoa yenu. Tatizo kubwa ni yale matatizo yanayomfanya mwenzi wako ajione anadhurumika kimapenzi hapo ndipo huwa hapatoshi.
 
MUME SIO BABA YAKO AKUNG'ANG'ANIE AU MKE SIO MAMA YAKO AKUNG'ANG'ANIE Pls listen to your heart, days are numbered

kuna ruba ndugu yangu wala usipime. tuulize tuliong'ang'aniwa hadi tukavunja simu na ilipobidi tukafika polisi. listening to your heart makes you a bit soft. just reasoning and thinking. the heart will follow
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…