Nyundo_tz
JF-Expert Member
- Jul 14, 2009
- 640
- 20
</SPAN>
Mwanaume mmoja nchini Saudi Arabia ambaye aliwabaka watoto watano miongoni mwao akiwemo mtoto wa kiume mwenye umri wa miaka mitatu ambaye alimtelekeza jangwani afariki, amehukumiwa kunyongwa na kisha mwili wake kuwekwa kwenye msalaba.
Mahakama nchini Saudi Arabia imemhukumu mwanaume aliyewabaka watoto watano adhabu ya kunyongwa na kisha mwili wake kuwekwa kwenye msalaba na kisha kuwekwa hadharani watu waushuhudie.
Mwanaume huyo mbali ya kuwabaka watoto hao watano, alimchukua mtoto mmoja wa kiume aliyembaka na kumtelekeza katikati ya jangwa ili afariki mwenyewe.
Mahakama ya rufaa ya mjini Riyadh imethibitisha adhabu hiyo ambayo ilitolewa mwezi juni mwaka huu na mahakama moja ndogo ya mji wa Hail ambako mwanaume huyo mwenye umri wa miaka 22 alifanya unyama wake huo,limeripoti gazeti la Okaz la Saudi Arabia.
Baada ya kunyongwa mbele ya hadhara, mwili wake utawekwa kwenye msalaba na kuwekwa wazi kwenye hadhara watu waushuhudie.
Mwanaume huyo ambaye hakutajwa jina lake, alikamatwa wiki chache zilizopita baada ya kujaribu kumlaghai mtoto mwingine kwa kumpa lifti ya baiskeli kutoka nyumbani kwao hadi shuleni kwao.
Jumla ya watu 56 wameishauliwa kwa kunyongwa mwaka huu nchini Saudi Arabia kutokana na makosa mbali mbali ya mauaji, ubakaji, ujambazi na usafirishaji wa madawa ya kulevya.
Watu wanaofanya mauaji ya kikatili hunyongwa na kisha miili yao kuwekwa kwenye hadhara.
Source: Reuters