Mbali na simba hakuna timu VPL iliyofikia kiwango cha Pamba ya Hussein Masha na George masatu

pamba boy

Senior Member
Joined
Jun 26, 2013
Posts
181
Reaction score
266
Nimeangalia ligi kuu ya Tanzania muda mrefu sana lakini hadi sasa hakuna timu iliyofikia kiwango cha uchezaji mpira wa kuvutia kama walivyokuwa pamba ya mwanza tp lindanda ya miaka ya 1990's ,ni simba tu ndiyo inaonyesha taswira halisi ya mpira wa enzi hizo!

Kiukweli kama kuna mtu alishuhudia mpira wa kina Hussein masha, George masatu, Mao mkami, Paul Rwechungura nk hakika soka la sasa la timu kama Yanga, Ihefu, Mbeya city, Coastal Union, JKT Tanzania, Namungo nk unaweza lifananisha na timu za daraja la tatu enzi hizo kama Lumumba rovers, coop united, Mandela fc, Toto African nk!
 
Napata picha hujawahi kuwaona ata ao pamba, Pamba ilikua timu sumbufu tu na haijawahi kubeba ubingwa wa Tanzania bara na haijawahi kuwanyima watu usingizi ni Kama Mecco walivyo panda au Tukuyu Tena Bora ya Tukuyu walipanda na kubeba ubingwa.
 
Wakati huo timu hizo zilikuwa na wachezaji wa nyumbani tu na kweli walisakata kabumbu safi kabisa lakini Simba hii ya sasa unakuta majority ya first XI ni wageni watupu.
 
Umemsahau mtangazaji aliyekuwa anawapamba sana Wana TP Lindanda, marehemu Dominick Chilambo
 
Umemsahau mtangazaji aliyekuwa anawapamba sana Wana TP Lindanda, marehemu Dominick Chilambo
Umemsahau mtangazaji aliyekuwa anawapamba sana Wana TP Lindanda, marehemu Dominick Chilambo
dah umenikumbusha mbali sana, walikuwa na shabiki yao muendesha baiskeli maarufu kama mang'ombe
 
Wakati huo timu hizo zilikuwa na wachezaji wa nyumbani tu na kweli walisakata kabumbu safi kabisa lakini Simba hii ya sasa unakuta majority ya first XI ni wageni watupu.
Lakini wanakuwa ni wa Simba au ugenini?
 
Napata picha hujawahi kuwaona ata ao pamba, Pamba ilikua timu sumbufu tu na haijawahi kubeba ubingwa wa Tanzania bara na haijawahi kuwanyima watu usingizi ni Kama Mecco walivyo panda au Tukuyu Tena Bora ya Tukuyu walipanda na kubeba ubingwa.
Nadhani uko sahihi alihadithiwa au alikuwa anasikia mapambo ya Marehemu Dominic Chilambo aliyeifanya Pamba ipambwe na ipambike kwa majina ya TP Lindanda Wana Kawekamo. Zaidi ya hapo Pamba ilikuwa timu sumbufu uwanjani kama Reli kiboko ya Vigogo ikiwa na akina Madundo Mtambo msomi ambaye kwa sasa ni Profesa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…