Mbao wanavuna walichokipanda, walifanya kosa la kwanza kumfukuza Ndailagije wakapata bahati ya kumpata Amri Saidi wakarudia kosa wakamuondoa

Mwakipizo

Member
Joined
Nov 6, 2019
Posts
25
Reaction score
16
Mbao wanavuna walichokipanda. Walianza kufanya makosa kwa kumfukuza ndailagije aliekua akiijenga timu taratibu wakapata bahati wakampata Amri Saidi akaanza na timu vizuri.

Sijui wakawaza nini wakafanya kosa lingine kwa kumletea Ali Bushiri kocha mzoefu aliemzidi elimu ya ukocha eti awe msaidizi wake, akaona anafukuzwa bila kuambiwa akaondoka. Baada ya Amri Saidi kuondoka tu, akaanza kupokea vichapo mpaka hapa walipofika hawana wa kumlaumu zaidi ya kujilaumu wenyewe.
 
Hakuna mkato, hakuna nukta, umeandika habar kama una kimbizwa.
 
Inaonekana hata hufatilii soka vizuri bali unadandia dandia tu mambo.

Ndayiragije hakufukuzwa Mbao bali KMC walipanda dau wakamnyakua, akaing'arisha KMC hapo napo Azam wakampandia dau akaondoka!!!
 
Wewe hufuatili ndio maana malalamiko ya mashabiki wa Mbao hukuyasikia
 
Inaonekana hata hufatilii soka vizuri bali unadandia dandia tu mambo.

Ndayiragije hakufukuzwa Mbao bali KMC walipanda dau wakamnyakua, akaing'arisha KMC hapo napo Azam wakampandia dau akaondoka!!!
Kwanza nikujuze tu kabla dailagije ajaenda KMC alishakubaliana na Singida United, KMC wakapanda dau kuliko la Singida
 
Pengine huelewi mizizi ya Uchafu katika Ligi Kuu ya Tanzania Bara tatizo mojawapo ambalo ni kubwa ni Ukata wa Pesa unaosababisha Timu ndogo kuuza Mechi ( ndio timu nyingi tu huuza mechi ili wapate pesa za kufanya mambo mengine) hata Mbao Football Club wanafamya sana huo mchezo nadhani mwaka huu hawakuchanga Karata zao vizuri ngoja washuke tu!
 
Mbao wanavuna walichokipanda. Walianza kufanya makosa kwa kumfukuza ndailagije aliekua akiijenga timu taratibu wakapata bahati wakampata Amri Saidi akaanza na timu vizuri.

Sijui wakawaza nini wakafanya kosa lingine kwa kumletea Ali Bushiri kocha mzoefu aliemzidi elimu ya ukocha eti awe msaidizi wake, akaona anafukuzwa bila kuambiwa akaondoka. Baada ya Amri Saidi kuondoka tu, akaanza kupokea vichapo mpaka hapa walipofika hawana wa kumlaumu zaidi ya kujilaumu wenyewe.
Ndayilagije hajawahi kufukuzwa Mbao,KMC na Azam ,huwa anapata dili kubwa anaondoka.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom