Wilaya ya Mbarali inasikitisha kuona barabara ina zaidi ya miezi nane hadi kumi, ikiwa imewekwa vifusi na havijasambazwa kwa kipindi cha muda mrefu.
Ni kama imetelekezwa pasipo kuendelezwa ujenzi wake hivyo kupelekea usumbufu kwa watumiaji wa njia hiyo, ikiwa ndio njia kuu kutoka Igawa kuelekea Ubaruku kupitia Rujewa.
Barabara hiyo ni mbovu na finyu yenye viraka vingi, yenye mashimo mengi kupelekea uharibifu wa vyombo vya usafiri na ajali wakati mwingine.
Inashangaza kuona Hali hiyo wakati huo njia hiyo inatumika na watu wengi na shughuli nyingi za uzalishaji na kiuchumi wilaya ya Mbarali.
Wahusika wanashindwa kulifanyia kazi jambo hili kwa kipindi kirefu tunashindwa kujua nini hatima yake!
View attachment 3337258View attachment 3337259View attachment 3337261View attachment 3337262View attachment 3337260