Mbaraza Kachebonaho akabidhi pikipiki tatu kwa UVCCM Temeke

Mbaraza Kachebonaho akabidhi pikipiki tatu kwa UVCCM Temeke

Pfizer

JF-Expert Member
Joined
Mar 25, 2021
Posts
590
Reaction score
807
IMG_20240415_082829_930.jpg

Mjumbe wa baraza Kuu Taifa Ndugu Leodger Kachebonaho Mapema Leo amekabidhi Pikipiki tatu zenye thamani ya shilingi 9,900,000 (Milioni tisa na laki tisa) Kama mradi wa UVCCM WILAYA YA TEMEKE.

Katika Hafla ya makabidhiano hayo yaliyofanyika Aprili 14, 2024 katika Ofisi za CCM (W) TEMEKE , Ndugu Kachebonaho aliwataka vijana Hao kupuuza kauli zinazokatisha tamaa vijana juu Ya kazi Ya Afisa Usafirishaji maarufu Kama bodaboda kwani bodaboda ni ajira rasmi na vijana wengi wamejiajiri na kuendesha Maisha yao kupitia kazi hiyo.

Akiongea katika hafla hiyo Ndugu Kachebonaho alisema “Nimetoa pikipiki ikiwa ni kujikuza kiuchumi kwani Jumuiya Imara ni ile ambayo inakuwa vizuri kiuchumi na viongozi wake wataweza kuendesha vikao vyao ndani kwa muda na pia kufanya shughuli mbalimbali za kisiasa katika jamii”

Pikipiki hizi zilizokabidhiwa leo ni Ahadi ya Ndugu Kachebonaho alipoalikwa Kuwa mgeni Rasmi katika kufunga baraza la UVCCM TEMEKE Mwezi februari Mwaka Huu.

Hata hivyo Ndugu Kachebonaho alitoa wito kwa viongozi vijana nchini kuacha alama Ya uongozi pale wanapopewa dhamana na vijana wenzao au jamii Kwani jambo Hili litaendelea kufungua fursa Ya vijana kuaminiwa katika nyanja mbalimbali katika Ujenzi wa Taifa letu.
 
Back
Top Bottom