Mbaroni kwa kutishia kuua kwa bastola

Mbaroni kwa kutishia kuua kwa bastola

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2012
Posts
5,108
Reaction score
10,191
MFANYABIASHARA, Adelard Lyakurwa (58), anayefanya shughi uli zake Kariakoo amepandishwa katika kizimba cha Mahakama ya Wilaya ya Ilala kujibu shtaka moja la kutishia kumuua mfanyabiashara mwenzie marufu, Valence Lekule kwa silaha, Bastola

Katika hati ya mashtaka iliyosomwa mahakamani hapo na wakili wa Serikali, Aziza Mhina mbele ya Hakimu Mfawidhi Martha Mpaze, imedai, Julai 30,2020 huko katika maeneo ya Kariakoo katika mtaa wa Mbaruku na Swahili iliyopo Wilaya ya Ilala Mkoani Dar ss Salaam, mshtakiwa Lyakurwa akiwa na lengo la kuua, alimtishia Valence Lekule kumuua kwa kutumia bastola huku akijua kuwa kufanya hivyo ni kosa na ni kinyume na kifungu cha 89 (2)(a) cha sheria ya kanuni ya adhabu sura ya 16 iliyofanyiwa marejeo mwaka 2019.

Hata hivyo, mshtakiwa Lyakurwa amekana kutenda kosa hilo na amerudishwa rumande baada ya kushindwa kutimiza masharti ya dhamana ambapo mahakama imemtaka kuwa na wadhamini wawili ambao watakuwa na barua zinazotambulika kisheria na kusaini bondi ya Sh. Milioni moja.

Kwa mujibu wa upande wa mashtaka upelelezi wa kesi hiyo umekamilika na wameomba ipangiwe tarehe nyingine kwa ajili ya kumsomea mshtakiwa maelezo ya awali.

Kesi hiyo imeahirishwa hadi Juni 2,2021 itakapokuja kwa ajili ya kusomewa maelezo ya awali.

Michuzi Blog
 
Maelezo uliyotoa ni ya kujilinda umepewa unaitumia kutisha tisha watu. Pathetic.
 
Katishia tu huyo inawezekana aliyetishiwa anadaiwa.
 
Julai 30,2020
Hata hivyo, mshtakiwa Lyakurwa amekana kutenda kosa hilo na amerudishwa rumande baada ya kushindwa kutimiza masharti ya dhamana ambapo mahakama imemtaka kuwa na wadhamini wawili ambao watakuwa na barua zinazotambulika kisheria na kusaini bondi ya Sh. Milioni moja.
Hapa kuna zengwe mahakamani July 2020 hadi leo!!!

Anyway mfanyabiashara Kariakoo anakosa wadhamini wa bond ya sh 1M!!!, huyo ndugu huenda ni mtata haishi na wenzake vizuri au hatabiriki, wanaweza wakamdhamini kesho akawalipua risasi
 
Kosa la kijinga kweli, katishia? Si angepiga kabisa? Watani zangu wana mambo halafu ni Lyakurwa na Lekule! Wacha niagize bia nisubirie mwandamo wa mwezi mimi
 
Hapa kuna zengwe mahakamani July 2020 hadi leo!!!

Anyway mfanyabiashara Kariakoo anakosa wadhamini wa bond ya sh 1M!!!, huyo ndugu huenda ni mtata haishi na wenzake vizuri au hatabiriki, wanaweza wakamdhamini kesho akawalipua risasi
Ukipandishwa mahakamani kama unajua kesi yako kuna kwenda selo lazima ujipange!
Mapema na mambo ya wadhamini,documents kadhaa,pesa
Ukienda kichwa kichwa utaenda siku 14 kimasihara

Ova
 
Kwa nn July 2020/halafu kesi inakuja kupelekwa mahakaman hv karibuni
 
Mkuu nakujibu kwa uzoefu wangu na yale yaliyonikuta.

Kesi imekaa zaidi ya miezi 8 na ni kesi ya ajabu mpaka kesho nashangaa wale watu walikuwa wanataka nini kwangu.

Ukimuuliza mpelelezi anakuambia mwanasheria wa kutoa majibu kuhusu kesi yako kuisha au inaendelea ana mambo mengi na hayupo kusubiri kesi yako, kesi zipo nyingi hivyo endelea kusubiri. Dah nilichukulia kawaida labda ndani ya wiki chache majibu yatakuwa tayari. Mzee zimekata miezi nikipiga simu naambiwa mwanasheria kasafiri yupo Dodoma hivyo mpka arudi Dar, na haijulikani lini.

Napiga simu tena naambiwa mwanasheria anaumwa hivyo niendelee kusubiri.

Unapiga siku nyingine unaambiwa suala la ofisi ya mwanasheria haikuhusu na utafahamishwa majibu yakiwa tayari. Nikiuliza lini? Naambiwa subiri utafahamishwa.

Danadana ziliendelea mpaka miezi zaidi ya nane kukatika .

Sasa hiki ndicho kinachosababisha hicho unachokishangaa kutokea mkuu.

Ofisi ya mwanasheria inaumiza wengi sana na ukipewa majibu suala lako liishie polisi, huwezi lipwa fidia na muda uliopoteza.

Mkuu ni usumbufu kupita kiasi. Ila toa pesa uone linavyoenda fasta. Rushwa haiwezi kuisha hii nchi. Nilikomaa sitoi kitu kabisa.

Kiufupi mkuu kuna watu wanateseka na kuumia sana kutokana na kinchofanywa ofisi za wanasheria wa serikali kwa kuchelewesha majibu.

Mkuu omba Mungu yasikutokee.

Kesi July 2020 inasikilizwa 2021, huo ni mchango wa ofisi za wanasheria kuchelewesha majibu kwa sababu za ajabu, sasa fikiria yule aliyenyimwa dhamana anateseka vipi. Inauma mzee.
 
mshtakiwa Lyakurwa akiwa na lengo la kuua, alimtishia Valence Lekule kumuua q

Michuzi Blog
Nia ya kuua, kosa la kutishia.

Ukishitakiwa kwa tendo la kutishia (actus reus) lazima pia nia ama lengo (mens rea) liwe kutishia.

Hati ya mashtaka hovyo, lakini mwandishi mwenyewe michuzi, you never know.
 
Back
Top Bottom