Msongoru
JF-Expert Member
- Apr 16, 2008
- 306
- 24
na Shangwe Thani, Shinyanga
JESHI la Polisi mkoani Shinyanga, linawashikilia walimu wawili wa shule za msingi kwa tuhuma za kuwafanyia mtihani wa taifa wa kumaliza elimu ya msingi wanafunzi watano kinyume cha sheria na taratibu za mitihani.
Kamanda wa Polisi mkoani Shinyanga, Shaibu Ibrahim, alisema ofisini kwake jana kuwa tukio hilo lilitokea Septemba 11 wakati wanafunzi wa shule za msingi nchini wakifanya mtihani wa taifa wa darasa la saba.
Aliwataja walimu wanaoshikiliwa na polisi kuwa Bengwe Hiellele (44), mwalimu wa Shule ya Msingi ya Ibango, iliyopo katika Kijiji cha Salawe Wilaya ya Shinyanga Vijijini na Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi ya Itobanilo, John Madirisha.
Mwalimu Hielele, aliyekuwa msimamizi wa mtihani katika shule hiyo kwa kushirikiana na mwalimu Madirisha ambaye ni mwalimu mkuu wa Shule ya Itobanilo, wanadaiwa kuwafanyia mtihani wanafunzi watano, kinyume cha sheria na taratibu za mitihani.
Kamanda Ibrahim, aliwataja wanafunzi waliofanyiwa mitihani kuwa ni Shangaluka Msala, Frank Jumanne, Maganga Magadya, John Jumanne na Saidi Cosmas na kwamba uchunguzi wa awali wa polisi umebaini kuwa wanafunzi hao walitoa shilingi 20,000 kila mmoja ili wasaidiwe kufanyiwa mtihani na walimu hao.
Alibainisha kuwa kabla ya kukamatwa kwao walimu hao walikuwa wamewafanyia mitihani ya hisabati, Kiswahili, Sayansi na Kiingereza na mwalimu Hielele, alipopekuliwa mfukoni alikutwa akiwa na karatasi ya maswali ya somo la hisabati ambao ulifanyika Septemba 10 mwaka huu.