Uchaguzi 2020 Mbatia v/s Mrema nani zaidi?

Uchaguzi 2020 Mbatia v/s Mrema nani zaidi?

lendila

JF-Expert Member
Joined
Sep 26, 2012
Posts
5,806
Reaction score
4,370
Mbatia v/s mrema nani zaidi?

Mrema na Mbatia wanafanya siasa zinafanana na wanatoka jimbo moja la vunjo

Mrema na Mbatia lengo lao sio kushika dola,lengo lao ni kuwa vyama vya upinzani maisha yao yote hili kalisema mbatia mwenyewe kuwa mwaka huu malengo yao Kama chama ni nini

Mrema na Mbatia hawana shida kabisa na kushika dola hili nalo hawalifichi kabisa wanasema wazi mchana kweupe

Lengo lao kubwa ni kushiriki chaguzi tu,na kupata kura au kugawa kura za wapenda mabadiliko

Swali,ni je kati ya Mrema na Mbatia nani ambaye mwaka 2020 atazichanga karata zake vizuri za kupata angalao kura nyingi kidogo kuliko mwenzake?

Nani atamdi mwenzake kwa kupata madiwani wengi kuliko mwenzake?
 
Wote hakuna mwenye afadhali

In God we Trust
 
Kuwapigia kura watu kama awo nibora nimpe Mgombea wa ccm , maana sioni utofauti wa Nccr na Ccm wala Tlp na ccm.
 
Huwezi umelinganisha hawa kwa kuwa mmoja ana mtafaruku wa jinsia (sexual disorder) wakati mwingine ni RIJALI hasa.
 
Bila kuwa na mgombea Uraisi hata kupata madiwani ni ndogo maana na wao badala ya kunadi wagombea wao watakuwa wanapambana kivyao kupata Jimbo
 
Hao wote ni CCM wakala, na hata teuzi huwa hawakosi.... kuna mwaka Mbatia aliteuliwa ubunge na JK na sasa Mrema kala shavu kwa JPM.

Wameshiriki ‘kupoza’ upinzani.
 
Wote wanagombea ubunge jimbo la vunjo lakini watagaragazwa vibaya sana na mwanamama Grace Kiwelu wa chadema.
 
chadema wabaya sana
Kawe walimpelekea mbatia mwanamke halima mdee akampiga chini
Chadema hao hao wanampelekea tena mwanamke shupavu kiwelu kushindana na mbatia vunjo
Kwanini chadema wanapenda kumshindanisha sana mbatia na wanawake?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mbatia anaweka historia kwa mara ya 2 kushindana na mwanake katika uchaguzi wa Jimbo
Je atavunja historia ya kumshinda mwanamke?
Mwaka 2010 alishindwa vibaya sana na mwanake halima mdee

Sent using Jamii Forums mobile app
 
chadema wabaya sana
Kawe walimpelekea mbatia mwanamke halima mdee akampiga chini
Chadema hao hao wanampelekea tena mwanamke shupavu kiwelu kushindana na mbatia vunjo
Kwanini chadema wanapenda kumshindanisha sana mbatia na wanawake?

Sent using Jamii Forums mobile app
Ni mwenzao , mwanaume suruali
 
Back
Top Bottom