MBC DRAMIA: Sehemu ambayo Wakorea wanafanya maajabu yao

MBC DRAMIA: Sehemu ambayo Wakorea wanafanya maajabu yao

Tea Party

JF-Expert Member
Joined
Oct 5, 2019
Posts
658
Reaction score
1,133
Ukiwa unaangalia series za kikorea za kihistoria kama JUMONG, SIX FLYING DRAGONS, EMPRESS KI au MR SUNSHINE kuna zile location za zamani ambazo huwa zinatumika.

Kuanzia kwenye jumba la kifalme (Palace), sokoni au kwenye makazi ya kawaida ya watu sehemu zote zinakuwa ni za kizamani kwenye enzi za Goryeo au Joseon. Binafsi nilipokuwa naangalia series nikawa najiuliza hizi sehemu zipo kweli hapa duniani?

Na kama zipo ziko wapi? Na je zile nyumba za kifalme ni za kweli au wanaigizia kwenye makumbusho? Na kama ni makumbusho watakuwa wanalipa shingapi? Ikabidi nianze uchunguzi wangu. Na hapo ndipo nikakutana na MBC DRAMIA.

MBC DRAMIA ilikamilika mwaka 2005 baada ya kituo cha TV MBC kuona haja ya kuanzisha studio zake makhususi kabisa kwa ajili ya kutengeneza historical dramas

Studio hii ya MBC DRAMIA ina total area ya 2,500,000 metres square.

Ndani ya MBC dramia kuna majengo ya kihistoria kutokea enzi za Goryeo, Samguk na Joseon.

Jina la MBC dramia limetokana na muunganiko wa neno "drama" na "utopia" ikatengeneza neno Dramia. Baada ya studio hii kuanza kupokea watalii mwaka 2015 ikabadilishwa jina kuitwa Yongin Daejanggeum Theme Park kwa sababu za kibiashara.

Series nyingi zilizotengenezwa MBC dramia ni kama MOON EMBRACING , GREAT QUEEM SEONDOK, DONG YI, MOON LOVERS nk.

MBC dramia inapokea watalii pia. Na kiingilio ni won 7000 kwa mtu mzima ambayo ni sawasawa na 14,000 za kibongo huku wanafunzi na watoto ni won 4500 sawasawa na 9000 za kibongo.

Pia kwa wale watalii ambao wangependa kupiga picha wakiwa wamevaa mavazi ya kikorea wanapewa heshima hiyo ambapo kukodisha Hanbok au "mavazi" ya kikorea ili kupiga, nayo picha ni won 40,000

Hiyo ndio MBC dramia.

Uzi tayari

this-is-korea-private.jpg
caption.jpg
af0a4125-20ab-4e40-9a7f-a0e8976aa274.jpg
001.jpg
 
Crowned clown..
Gu family Book
...Kings doctor .. zilishutiwa hapo..
Rebel thief.. Who stole people's heart.
♥️♥️♥️♥️♥️♥️
 
Crowned clown..
Gu family Book
...Kings doctor .. zilishutiwa hapo..
Rebel thief.. Who stole people's heart.
[emoji3531][emoji3531][emoji3531][emoji3531][emoji3531][emoji3531]
Kabisa mkuu
 
Back
Top Bottom