mrdocumentor
Member
- Nov 27, 2021
- 45
- 56
Msitu tunaoishi ni msitu wenye mandhari nzuri sana na ya kuvutia umepambwa na ukijani unaoelekea kuwa weusi kutokana na udongo mzuri na wenye rutuba unaopatikana katika msitu huu wa Amani.
Katika msitu huu wa Amani kuna kila kitu ambacho sisi kama wakazi wa msitu huu tunakihitaji. Mfano Matunda mazuri na Matamu yanapatikana katika msitu huu ambayo hutumika kama chakula kwetu lakini pia katika msitu huu yapo matunda ambayo hayapatikani katika msitu wowote duniani isipokuwa katika msitu wetu wa Amani tu.
Tuliamua kuupa msitu wetu jina la Amani kwa sababu Wanyama wengi tuishio katika msitu huu ni wakarimu na wapenda amani jambo ambalo linafanya hata wanyama wengine kutoka misitu mingine ya jirani na ya mbali kukimbilia msituni kwetu kutafuta hifadhi pale wanapopata matatizo.
Picha kutoka mtandaoni
Jambo jingine la kufurahisha katika msitu wetu huu tunaishi wanayama wa aina moja tu.
Sisi sote ni Mbega tunaishi kama jamii moja richa ya kuwa tunatofautishwa na rangi zetu tu ambazo hutugawa katika makundi mawili ambayo ni Mbega weusi na mbega wekundu.
Katika kuishi kama jamii moja yenye makundi Mawili mahusiano yetu katika kuishi uku yamegawanyika katika zama mbalimbali kulingana na wakati zipo nyakati tuliishi kwa amani na zipo nyakati tuliishi kwa shida na kutoelewana.
Ngoja nikupe kidogo historia ya mahusiano yetu uko nyuma hadi zama za sasa.
Mimi ni Mbega mweusi ambae nmepata bahati ya kuishi katika msitu huu wa amani kwa miaka mingi na zama nyingi sana zimepita na mimi zikiniacha kushuhudia zama zingine. Katika zama hizo zote nimeshuhudia matukio mengi sana yahusuyo mahusiano yetu sisi na Mbega wekundu
Ni ukweli usiopingika kuwa hapo zamani kundi letu la Mbega weusi tulikuwa tukiwanyanyasa na kuwadhalilisha sana mbega wekundu
Katika zama za nyuma Mbega mwekundu alikuwa anaishi katika msitu huu kama mgeni tu na akawa mtumwa wa mbega weusi kwa wakati ule. Ilifikia hatua hakuwa na haki yoyote katika msitu huu ijapokuwa ni mkazi wa msitu huu.
Wakati Mbega weusi wadogo wakipewa mafunzo ya namna bora ya kutafuta matunda na chakula, Mbega wekundu wao hawakujumuishwa katika mafunzo hayo.
Hali hiyo ilizidi kudidimiza haki za Mbega hao wekundu na kufifisha matumaini kabisa ya wao kupata haki zao kwa sababu ikiwa mtu unamnyima mafunzo au mbinu za kutafuta chakula moja kwa moja unamfanya awe tegemezi kwako na utamfanya utakavyo kwa sababu kula yake inatokana na Wewe.
Hata kama Mbega wakaadhimia kuwa na kikao cha kujadili mambo mbalimbali basi Mbega weusi pekee ndo wataruhusiwa kuchangia uku wekundu wakibaki kama wasikilizaji tu na kufuata yale wakatakayokubaliana Mbega weusi. Hakika tuliwatenga, tuliwadhalilisha na kuwanyanyasa ndugu zetu hawa.
Hakuna Mbega mwekundu yeyote aliyekuwa na uhuru wa kufanya chochote kilichopo ndani ya moyo wake au ndani ya matamanio ya nafsi yake pasi na idhini ya Mbega weusi kwa maana matamanio ya nafsi za Mbega wekundu yalikuwa kwenye viganja vyetu aidha tuyafinye au tuyaachie
Bado haikutosha ilikuwa hakuna Mbega mwekundu yeyote aliyeruhusiwa kuongoza msafara hata wa Mbega wawili kwenda kutafuta chakula wao walikuwa ni wafuataji tu msafara au watabaki nyumbani wasubiri kuletewa kidogo tutakachopata. Na ikitokea kuna Mbega mwekundu amejaribu kufanya hivyo basi adhabu yake ni kali mno.
Mbega wekundu walipitia hayo mateso kwa muda mrefu sana na walishindwa kabisa kufurahia mandhari na uzuri wa msitu huu wa Amani. Jina hili la msitu wa Amani kwao halikuwa na maana yoyote kwa sababu hakukuwa na amani hata chembe kwa upande wao.
Picha kutoka mtandaoni
“Hakuna marefu yasiyo na ncha”
Wahenga walikuwa sahihi sana. Mbega wekundu ilifika hatua wakajiuliza “haya mateso hadi lini” ukizingatia hawakuwa na mahali pengine pa kukimbilia zaidi ya kubaki pale.
Baada ya kukaa na kushauriana kwa dakika kadhaa walikubaliana kudai haki zao na kutaka amani katika msitu huu wa Amani. Walihamasishana na kupeana njia zitakazowafanya wafikie lengo lao kwa taratibu lakini kwa ufanisi zaidi.
Waliwaeleza Mbega weusi malalamiko yao na madai yao ya kutaka kuonja amani ya msitu huu. Richa ya nidhamu na jitihada walizotumia lakini bado Mbega weusi hawakuonesha dalili za kukubaliana na mawazo yao. Kiufupi jitihada zao ziligonga mwamba.
Hawakukata tamaa bado waliendelea kuomba na kuomba zaidi hadi ikafikia hatua ya kudai haki zao kwa lazima.
Mbega wekundu waliendelea kuwashawishi mbega weusi kwa maneno matamu kwa kuwaambia kuwa ikiwa watakubali kumuweka huru Mbega mwekundu basi hata jamii yao pia itasonga mbele kwa haraka kwa sababu Mbega wekundu pia watakuwa Sehemu ya mchango wa utafutaji matunda na chakula kingine hivyo nguvu kazi itakuwa imeongezeka.
Wengi katika kundi la Mbega weusi walishawishika na maneno ya Mbega wekundu na wachache sana walibaki na Misimamo yao
Mbega wekundu walipata nguvu zaidi ya kupigania haki yao na kazi yao ilikuwa rahisi sana kwa mda huo kwa sababu upinzani ulikuwa mdogo sana.
Baada ya kuteka hisia za kundi la Mbega weusi na kuona njia ya kupata kile wanachokihitaji. Mbega hawa walianza jeuri na kiburi mapema tu na kujiona kuwa mafanikio yale ni ya kwao wenyewe wala sisi hatukushiriki katika hilo, hali ya kuwa wapo Mbega weusi wengi ambao walisaidia katika harakati hizo. Wakaanza sasa kuweka misingi yao na kulazimisha kujifananisha na Mbega weusi richa ya baadhi ya vitu kuwa hatuwezi kufanana Kamwe.
Mbega wekundu sasa wanalia kivulini
Zimefika zama hizi za sasa ambazo Mbega wekundu wameshajikomboa kutoka kwenye unyanyasaji na udhalilishaji sasa wanaaminiwa, wanasikilizwa, wanapendwa na wanapata kila kitu wanachokihitaji kutokana na matamanio ya nafsi zao.
Kwa sasa Mbega wekundu wana uwezo wa kuongoza kundi kubwa la Mbega wekundu au weusi na wakaenda mawindoni kutafuta chakula.
Mbega wekundu waliongoza misafara mbalimbali katika msitu na makundi mbalimbali ili waweze kurudi na chakula kwenye makazi
Walifanya vizuri kazi zao tena sana hadi tukajisemea wenyewe kuwa tulichelewa sana kuwaamini hawa viumbe hakika msitu wetu ungekuwa na baraka toka zamani.
Richa ya uchapakazi wao lakini tatizo kubwa la mbega wekundu lilikuwa kutaka kuwaaminisha kwa haraka Mbega weusi kuwa wao wekundu ni bora kuliko wengine na wanaweza kufanya zaidi ya Mbega weusi.
“Hapa ndipo walipokosea”
Matokeo ya kufanya hivyo wakajikuta wanachukua matunda hata ambayo hayajakomaa na kuleta kwenye makazi lakini pia Mbega wekundu walikuwa wanapora hata yale matunda machache ambayo wamepata wale wanaowaongoza ambayo yangewasaidia wao kwenye hiyo safari Lakini mbega wekundu wanachukua yale na kuyapeleka kwenye azina ya msitu Uku msafara wake ukisafiri na njaa na yeye wala hajali wala kusikiliza.
Mbega mwekundu angeweza kutafuta Sehemu tofauti za kupata matunda tofauti na yale ya anaowaongoza kwenye msafara ila kwakuwa anataka kuwaaminisha Mbega weusi kuwa yeye na wenzake ni bora kuliko wao inamlazimu afanye hivyo.
"Mbega wekundu wametugeuka"
Tulipokuja kushtuka tumeshachelewa Mbega wekundu tuliowasaidia wenyewe leo wametugeuka. Mbega mwekundu akiwa Sehemu yoyote basi atakuwa hapo kwa maslahi ya Mbega wekundu wenzake.
Unyanyapaa ukatanda kwenye msitu wetu wa Amani.
Wakajisahau! Wakasahau kabisa kuwa walikuwa wadhaifu kwetu. Tukawa watazamaji wa mwisho wake. Matokeo yake tunaanza kuyaona sasa wanajirudisha chini wenyewe na kutukabidhi kijiti chetu bila wao kujua.
Si hawa ambao walikuwa wanapinga udhalilishaji?.
Kwa sasa wanajidhalilisha wenyewe.
Anatokea Mbega mmoja anawashawishi wengine anapata kundi kubwa kwa pamoja wanashirikiana kumdhalilisha mmoja wao, wengine wanafurahi bila kujua kuwa yule mmoja wanaefurahia kumdhalilisha siku moja atakuwa ni yeye. Hayo yote ni matokeo ya kuwaweka huru. Hawasikii tena kwa bahati Mbaya wanahitaji msaada wetu zaidi japo wanajiona wanatosha ila sisi ni wa muhimu sana kwao.
Nikili kuwa hapo nyuma tulikuwa katika makosa sana kumnyima uhuru Mbega mwekundu ila kama ukitumia jicho la hekima zaidi utagundua kuwa kwa Sehemu kubwa tulikuwa sahihi na ndogo sana ndo tulikosea.
Kwa sasa msitu wetu umekosa amani kila Mbega analalamika Kila uchwao si weusi si wekundu wote wanapitia kipindi kigumu.
Acha tuwasubiri tu hapa chini wanashuka wenyewe na wakishuka hatuwapandishi tena.
Tamati
Upvote
6