Interesting!!Pia kama unataka matokeo mazuri nunua vifaranga ambavyo ni madume pekee (mono-sex) samaki madume wanakuwa haraka kuliko majike, ukifuga madume pekee utazuia population na kutengeneza mazingira mazuri kwa samaki wako kukuwa kwa haraka
Kimsingi vifaranga uzalishwa hatchery, tunakusanya vifaranga toka midomoni mwa majike tunapeleka hatchery kwenye incubator jar hapo mayai yanakaa kwa siku 1 - 3 vifaranga vinatotolewa,Interesting!!
Wanawatenganishaje vifaranga wadogo namna ile kama sisimizi
acha fiksi wewe hakuna sato mwenye kilo moja dunianiMbegu bora ya samaki ni ile inayozalishwa na wataalamu wa ufugaji samaki zipo taasisi zilizojikita kuzalisha mbegu ya samaki wa kufugwa kama vile Big fish, Eden agri-aqua, SUA n.k
Kwa uzoefu wangu mbegu nzuri kwa samaki aina ya sato ni Nile Tilapia (Oreochromis niloticus) hii ni specie nzuri samaki anaweza kufika hadi uzito wa 1kg - 2kg kama utamfuga na kumlisha vizuri
Pia kama unataka matokeo mazuri nunua vifaranga ambavyo ni madume pekee (mono-sex) samaki madume wanakuwa haraka kuliko majike, ukifuga madume pekee utazuia population na kutengeneza mazingira mazuri kwa samaki wako kukuwa kwa haraka
Karibu kwa ushauli na msaada zaidi kuhusu chochote kuhusiana na ufugaji samaki
Sijakuelewa hapa mkuutunakusanya vifaranga toka midomoni mwa majike tunapeleka hatchery kwenye incubator jar hapo mayai yanakaa kwa siku 1 - 3 vifaranga vinatotolewa,
Kimsingi vifaranga uzalishwa hatchery, tunakusanya vifaranga toka midomoni mwa majike tunapeleka hatchery kwenye incubator jar hapo mayai yanakaa kwa siku 1 - 3 vifaranga vinatotolewa,
Hatua inayofata inakuwa ni kuwapa dose ya kufanya wawe madume kwa siku 21 tunawapa hormone kwa ajili ya sex reversal
Nimejaribu kuelezea kwa ufupi zoezi la utotoleshaji wa vifaranga vya samakiSijakuelewa hapa mkuu
[emoji16][emoji16]acha fiksi wewe hakuna sato mwenye kilo moja duniani
Namashaka na uelewa wako kuhusu samaki, nimekuwa kwenye industry kwa zaidi ya miaka mitatu nimeshuhudia samaki wengi tu ambao wanazaidi ya kilo 1acha fiksi wewe hakuna sato mwenye kilo moja duniani
Nilichoandika na ushahidi nacho[emoji16][emoji16]
Kaongeza chumvi kidogo.
Ila kwa ufugaji wa samaki, haishauriwi ufuge samaki mpaka afike kilo 1 kwa sababu ya muda, soko, na gharama ya chakula.
Wafugaji wengi wa kisasa wanatoa samaki kwa miezi 6/7 akiwa na gramu 300-500 kilo moja unapata samaki 3-4. Kwa uzito huu ni rahisi hata kuwauzia watanzania wa kawaida wanao taka samaki wa 2000/3000/1500.
na useme ana miaka mingapi sio kusema kilo moja tu, sema ana miezi sita tukuchekeNilichoandika na ushahidi nacho
Huyu samaki anazaidi ya kilo moja, picha niliipiga mimi mwenyewe
Oh thanks sikujua hili, kujifunza hakuna kikomo mkuuSamaki sato ni aina ya samaki wanaotunza, kutolesha na kutunza vifanya wao mdomoni (mouth brooders)
Ili kuzalisha vifaranga ambao watakuwa na uniform size inakulazimu kukusanya mayai toka kwenye vinywa vya Samaki wazazi (egg robbery) na kupeleka kwenye incubator kwa ajili ya kuyatotolesha
Niweke sahihi, hoja ilikuwa hakuna sato mwenye kilo mojana useme ana miaka mingapi sio kusema kilo moja tu, sema ana miezi sita tukucheke
1. Sato ni samaki anaekula vyakula aina ya mimea na wanyama/wadudu (phytoplankton and zooplankton) ila kwenye ufugaji tunawalisha chakula chenye mchanganyiko wa virutubisho muhimu (pumba za mahindi, mpunga, mabaki ya dagaa, soya, mashudu ya alizeti n.k) usagwa, uchanganywa na kisha utengenezwa na mwisho samaki wanapewa kikiwa in pellet form ili kiweze kuelea juu ya maji wakati wa kulishaOh thanks sikujua hili, kujifunza hakuna kikomo mkuu
- Kwa utaratibu huo samaki mwenyewe anakulaje
- Nawe mtaalamu unatumia mbinu gani kuyapata hayo mayai kinywani mwa samaki wakati yuko majini
- Unamtambuaje kuwa yupo katika stage hizo
Barikiwa mtumishi, nimejifunza makubwa toka kwako1. Sato ni samaki anaekula vyakula aina ya mimea na wanyama/wadudu (phytoplankton and zooplankton) ila kwenye ufugaji tunawalisha chakula chenye mchanganyiko wa virutubisho muhimu (pumba za mahindi, mpunga, mabaki ya dagaa, soya, mashudu ya alizeti n.k) usagwa, uchanganywa na kisha utengenezwa na mwisho samaki wanapewa kikiwa in pellet form ili kiweze kuelea juu ya maji wakati wa kulisha
2 & 3. Samaki wazazi (brooders) uwa wanatengwa nakuwekwa kwenye Happa net kwa ratio ya majike wa 3 kwa dume mmoja na mayai yanakusanywa toka kwenye vinywa vya majike kila baada ya wiki mbili. Majike wenye mayai wanajulikana kwa tabia yao ya kupana midomo pindi unapomshika na taya zao zinakuwa zimejaa na pia wanakuwa very aggressive unapowatoa kwenye maji