Mbegu za Kiume za Beckham Kununuliwa kwa Euro Milioni 75

Ng'wanza Madaso

JF-Expert Member
Joined
Oct 21, 2008
Posts
2,268
Reaction score
335
Mbegu za Kiume za Beckham Kununuliwa kwa Euro Milioni 75
3632354.jpg

David BeckhamFriday, November 27, 2009 11:12 PM

Benki moja ya mbegu za kiume iliyopo California nchini Marekani iko tayari kununua mbegu za kiume za mchezaji nyota wa Uingereza David Beckham kwa euro milioni 75 kwaajili ya wanawake matajiri wanaotaka kupata watoto wanaofanana na watu maarufu.Wanawake matajiri wanaotaka watoto wanaofanana na watu maarufu duniani wameongezeka kwa wingi na kuifanya benki ya mbegu za kiume yenye makazi yake California nchini Marekani Cryobank ijaribu kununua mbegu za kiume za watu maarufu.

Cryobank inadaiwa kumfuata mchezaji nyota wa Uingereza anayesakata kabumbu nchini Marekani, David Beckham na kumshawishi awauzie mbegu zake za kiume kwa euro milioni 75.

Hata hivyo inadaiwa kuwa David Beckham alikataa dili hilo.

Cryobank mbali ya Beckham inadaiwa kuwafuata pia nyota kibao wa filamu wa nchini Marekani wakiwataka wachangie mbegu zao za kiume kwenye benki hiyo kwa malipo ya mamilioni ya Euro.

Mmoja wa nyota hao ni Brad Pitt aliyeambiwa atalipwa euro milioni 60 iwapo atachangia mbegu zake za kiume kwenye benki hiyo.

Mchezaji bora wa dunia Cristiano Ronaldo anayechezea timu ya Real Madrid ya Hispania naye yumo kwenye listi hiyo ya masupastaa na mbegu zake za kiume zinahitajika kwa euro milioni 50.

Cryobank kwa miaka 30 sasa imekuwa ikijishughulisha na upandikizaji wa mimba kwa wanawake kwa kutumia mbegu za kiume za watu wanaojitolea kwenye benki hiyo.

Cryobank imekuwa ikijiingizia mamilioni ya dola kutokana na kuongezeka kwa idadi ya wanawake wanaotaka kupata watoto kwa njia ya upandikizaji wa mbegu za kiume.

Source:Nifahamishe
 
Kuna mtu humu i think ni gorgie porgie
aliwahi kuja na mada ya kumpa mwanamke mbegu ili azae...
Nikamwambia wengine tuna asili ya pesa na utajiri..
So akisoma hii ataelewa.
 
hahaha The boss tetetete umenichekesha

sasa kale ka mama posh spicy katamruhusu akakamate hilo dili ?
 
Jamani mbona dili hilo halinikuti mimi?
beba maparachichi misha nenda pale ubalozi wa marekani Dar, wapigie kelele kwamba unataka kuwalipua. then utakuwa mtu maarufu ghafla halafu wanawake matajiri watataka mbegu zako wajidunge nazo (huku wewe unaozea guantanamo)
 
vitendo umaarufu unatafutwa hauji hivi hivi ndo maana kashauliwa achuku maparachichi akatest zali
 
Kuna mtu humu i think ni gorgie porgie
aliwahi kuja na mada ya kumpa mwanamke mbegu ili azae...
Nikamwambia wengine tuna asili ya pesa na utajiri..
So akisoma hii ataelewa.

kulikuwa na wakati wasichana wengi walipendezewa wapate watoto na waziri mkuu wa TANZANIA aliyekuwepo madarakni hivi sasa .
 
Kuna mtu humu i think ni gorgie porgie
aliwahi kuja na mada ya kumpa mwanamke mbegu ili azae...
Nikamwambia wengine tuna asili ya pesa na utajiri..
So akisoma hii ataelewa.

mmmmh the boss, naona hii topic umeifurahia kwelikweli.
haya bwana wenye pesa... lakini icje ikawa ni ufisadi vilevile
 
Mbegu za Kiume za Beckham Kununuliwa kwa Euro Milioni 75
3632354.jpg

David BeckhamFriday, November 27, 2009 11:12 PM

Benki moja ya mbegu za kiume iliyopo California nchini Marekani iko tayari kununua mbegu za kiume za mchezaji nyota wa Uingereza David Beckham kwa euro milioni 75 kwaajili ya wanawake matajiri wanaotaka kupata watoto wanaofanana na watu maarufu.Wanawake matajiri wanaotaka watoto wanaofanana na watu maarufu duniani wameongezeka kwa wingi na kuifanya benki ya mbegu za kiume yenye makazi yake California nchini Marekani Cryobank ijaribu kununua mbegu za kiume za watu maarufu.

Cryobank inadaiwa kumfuata mchezaji nyota wa Uingereza anayesakata kabumbu nchini Marekani, David Beckham na kumshawishi awauzie mbegu zake za kiume kwa euro milioni 75.

Hata hivyo inadaiwa kuwa David Beckham alikataa dili hilo.

Cryobank mbali ya Beckham inadaiwa kuwafuata pia nyota kibao wa filamu wa nchini Marekani wakiwataka wachangie mbegu zao za kiume kwenye benki hiyo kwa malipo ya mamilioni ya Euro.

Mmoja wa nyota hao ni Brad Pitt aliyeambiwa atalipwa euro milioni 60 iwapo atachangia mbegu zake za kiume kwenye benki hiyo.

Mchezaji bora wa dunia Cristiano Ronaldo anayechezea timu ya Real Madrid ya Hispania naye yumo kwenye listi hiyo ya masupastaa na mbegu zake za kiume zinahitajika kwa euro milioni 50.

Cryobank kwa miaka 30 sasa imekuwa ikijishughulisha na upandikizaji wa mimba kwa wanawake kwa kutumia mbegu za kiume za watu wanaojitolea kwenye benki hiyo.

Cryobank imekuwa ikijiingizia mamilioni ya dola kutokana na kuongezeka kwa idadi ya wanawake wanaotaka kupata watoto kwa njia ya upandikizaji wa mbegu za kiume.

Source:Nifahamishe

Upuuzi mwingine wa wazungu huu
 
Back
Top Bottom