Mbegu za Mahindi za Muda Mfupi

mayenga

JF-Expert Member
Joined
Sep 6, 2009
Posts
4,118
Reaction score
1,970
Wadau,

Nami nimeamua kujitosa kulima katika msimu huu, shamba alangu liko kisarawe, nahitaji mbegu za mahindi ambazo ni za muda mfupi kwani mwaka huu inaonekana mvua zitanyesha kwa muda mfupi.

Nilikuwa kama kuna agent au yeyote mwenye kuhusika na uuzaji wa pembejeo aweke mawasiliano yake hapa,hasa kwa wale walioko dar es salaam.
 
Nilipenda kweli kuchangia hapa lakini kwa sasa sina jibu zuri, ila mwisho wa mwezi huu hadi mwanzoni mwa machi kwenye tarehe kama tatu hivi nitakuwa na jibu la swali lako maana natarajia kwenda chuo cha kilimo Ilonga kupata ufafanuzi wa haya makitu.
 
Usinunue kariakoo sokoni ,mbegu nyingi pale feki.huko zinastawi star,situka2.pia mbegu za pannar ni nzuri sana kwa mfano pannar19 ni ya muda mfupi.wapo millenium park pale shekilango. Pia suba trading wapo mtaa wa akamba kariakoo.
 
Nilipenda kweli kuchangia hapa lakini kwa sasa sina jibu zuri, ila mwisho wa mwezi huu hadi mwanzoni mwa machi kwenye tarehe kama tatu hivi nitakuwa na jibu la swali lako maana natarajia kwenda chuo cha kilimo Ilonga kupata ufafanuzi wa haya makitu.

Kabla hujaenda unaweza kumtwangia huyu MAMA ndo anashughulika na kuuza Mbegu! MBEGU,mahindi pia kuna TMV na hawa jamaa wa SUBA wana Mbegu yao inaitwa kiFARU ni nzuri sana!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…