Mbegu za Mbono Kinga dhidi Ya Maradhi ya Majipu

Mbegu za Mbono Kinga dhidi Ya Maradhi ya Majipu

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2009
Posts
42,872
Reaction score
34,363
1388852_mbegu_za_mnyonyo-1024x768.jpg

MBEGU ZA MBONO AU MNYONYO
Mara nyingi katika mada zangu nimekuwa nikizungumzia namna ya kutibu maradhi mbalimbali yanayomkwamisha mwanadamu kushiriki ipasavyo kazi za ujenzi wa taifa.
Tiba ninazozungumzia ni zile asili zisizoacha athari mbaya kwenye mwili wa mgonjwa. Leo nimeona nizungumzie namna ya kujikinga dhidi ya majipu.

Kinga hiyo ni mbegu za nyonyo au mbono.
Chukua mbegu hizo, ni vema ziwe zile ndogo zenye ukubwa wa kidonge, meza moja asubuhi, moja mchana na nyingine jioni muda wa siku tano. Rudia dozi hii baada ya miezi minne. Hii ni kinga nzuri hususan kwa anayeotwa majipu mara kwa mara.
Majipu pamoja na kumsababishia mgonjwa maumivu makali pia yanamwacha na makovu ambayo huchukua miaka mingi kuondoka katika ngozi yake.
Kimsingi jipu au majipu husababishwa na vijidudu wanaojulikana kama ‘stafilokokasi’ ambao huingia kwenye vijifuko vya jasho kupitia vinyweleo vya mwili. Jipu ni uvimbe unaoanza sehemu maalumu.
Linaweza kuwa jipu moja au zaidi. Uvimbe wa jipu hukua na kisha kutunga usaa ambao hutumbuka. Mwanzo jipu huwasha na kisha huwa na maumivu makali hasa linapoota sehemu ambayo ngozi yake imebana kama puani , sikioni, kwapani au katikati ya kidole.
Mara nyingi chanzo cha jipu ni sumu ndani ya mfumo wa damu inayosababishwa na kutokula vyakula vinavyostahili mwilini
 
Back
Top Bottom