Robert Heriel Mtibeli
JF-Expert Member
- Mar 24, 2018
- 28,297
- 68,017
MBELE KUNA GIZA NENE, KULIA NA KUSAGA MENO!
Anaandika, Robert Heriel.
Njia imesonga, nuru inazidi kufifia, Kurudi nyuma haiwezekani, mbele nako giza limetanda, twajua tulipotoka lakini hatuna uhakika wa hatma yetu.
Pale nguvu zitakapotuisha, akili itakapo poteza uwezo wake wa kufikiri. Nini kitatokea, nani atawaza badala yetu, na Nani atatenda Kwa ajili yetu ikiwa mambo yenyewe mpaka sasa yapo hivi.
Ikiwa Sisi tuliolelewa Kwa upendo hatuwajali wazazi wetu, Fikiria hatukulelewa na Wafanyakazi WA ndani, mikono ya Mama zetu ndio ilitutunza, jasho la Baba zetu ndilo lilituogesha na kutupa nguvu ya kufika hapa tulipo. Lakini hatuwajali wazazi wetu.
Ikiwa tuliwaona Baba na Mama pamoja, tukawa familia Moja na ndugu zetu wa tumbo moja. Lakini leo hatuwajali.
Vipi leo ambapo kadiri siku zinavyosonga Sisi hatuwezi Kulea watoto wetu Kwa pamoja kama Mke na Mume, aidha mtoto alelewe na Baba au mara nyingi Mama, na hiyo Kama itashindikana atalelewa huko kwenye Daycare au Boarding school. Nini kitatokea tutapokaribia ukingo.
Tutakufa bila faraja, tutafumba macho yetu mbele ya watu tusiowajua, na pengine tutazikwa na adui zetu Kwa nyimbo Kama sherehe za Harusi.
Nani atakayetulilia, Nani atakayetukumbuka. Giza! Giza! Ndilo litatufunika, uchungu! Uchungu ndio utakaotumaliza.
Vilio na kusaga Meno navisikia gizani, ikiwa Mama wa leo aliyebeba watoto wa Baba mmoja lakini watoto hao hawasikilizani, haijulikani nani mkubwa na yupi nu mdogo, hawapendani, na Mama hasaidiwi na watoto wake aliowazaa, tena nikafikiri labda ni LAANA lakini nikakataa, nikasema pengine ni karma, pia nikakataa nikasema Kwa mara ya mwisho labda ndio mwisho wa Zama. Ikiwa Mama huyo anahangaika hivi leo, vipi Kwa Yule mama mwenye Watoto wa Baba tofauti tofauti, ambao kimsingi Zama hizi ndio wamejaa. Je watoto hao wa damu tofauti watasikilizana huko mbeleni tuendako? Kilio, Kilio! Kilio Kwa Wamama waliozaa.
Tena Baba Naye Mama siku ukiumwa unafikiri nini, au itakuwaje pengine tusubiri itakavyokuwa. Huko mbeleni lilipo Giza utauguzwa na usiowahi kuwadhani katika maisha yako, tena watakaokubadilisha nguo zako, na kukusafisha mwili na uchafu wako watakuwa watu usiowaona Kwa maana kutakuwa na Giza kuu. Watu ambao sio wadamu yako ndio Ndugu zako, wala hawatakuwa watoto wako uliowazaa wewe mwenyewe.
Watakaokulea na kukuuguza watatoka mbali usikokujua, na wala hutojua walikoelekea ndugu na watoto wako.
Utalala kitandani ukiwauliza watu hao, ndugu na watoto wangu hawajafika, utajibiwa bado hawajafika, utasema tena, Ndugu na watoto wangu hawajanitumia hata ujumbe, utajibiwa hawajatuma. Utakaa kimya ukitafakari na kutaka kujua habari za ndugu zako na watoto wako. Moyo wako utazimia sio Kwa sababu ya ugonjwa, mwili wako utadhoofu sio Kwa sababu ya kuugua Bali Kwa sababu ya kutengwa na kuachwa na watu wako katika Giza kuu.
Labda ungetamani kuwa hata Kero Kwa Ndugu na watoto wako lakini Hilo halitotokea, utakuwa kero Kwa watu usiowajua, na hilo litakuumiza, utahudumiwa na Wale uliowadharau na kuwaona sio kitu nyakati ulipokuwa na nguvu. Hilo litakukondesha na kutesa Nafsi yako. Dhamiri yako itakushtaki katika mahakamani ya Nafsi. Hukumu yako utaikubali lakini kesi haitotaka kuisha ili kukufanya ulipie deni la Dharau, kiburi na jeuri uliyoifanya katika nyakati za Nuru.
Kama vile ulivyothamini pesa kuliko UTU, ndivyo itakavyokuwa kipindi ukiwa na uhitaji, watu tena wale uliowategemea watathamini pesa kuliko UTU wako, utakuwa na pesa lakini hautazihitaji utakachohitaji ni faraja kutoka Kwa watu, lakini watu hawatakupa hizo faraja.
Familia hujengwa Kwa Roho na wala sio vitu. Ikiwa familia utajengwa Kwa vitu basi itabomolewa na vitu Kwa maana vitu vina expiredate. Siku vitu hivyo vitapo Expire ndipo na familia yako itakapoanguka.
Naliona Giza na anguko la familia zijazo Kwa sababu watu wengi wamejenga mahusiano Yao ya kifamilia katika Vitu mfano wa Pesa. Wasijue pesa ni sabuni ya roho lakini sabuni inapoisha huacha mapovu na takataka kwenye roho ambapo Bila maji ya kusuuza roho iliyosafishwa na sabuni"Pesa" basi Roho bado itabaki na dosari.
Maji ni Upendo, upendo ndio husuuza Nafsi ya mtu. Upendo ni Uhai Kama yalivyo maji.
Taikon akili yangu inaniambia kuwa, kwenye Giza kinachihitajika sio Nuru wakati wote, Bali macho ya kuona Kwa maana hata mtu akiwa kwenye Nuru Kama hana macho basi hawezi kuona. Hivyo nuru na Giza ni Sawa Kwa mtu aonaye, Kama vile ilivyo Nuru na Giza ni Sawa Kwa mtu asiyeona.
Acha nipumzike sasa,
Ni Yule Taikon kutoka Nyota ya Tibeli.
Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Safarini kuelekea Dar es salaam