Mbele kwa mbele- dj Yusuf ft. Hard Mard

Mbele kwa mbele- dj Yusuf ft. Hard Mard

Lyrics Master

JF-Expert Member
Joined
Apr 2, 2016
Posts
479
Reaction score
670
Verse 01:

Kipyenga kimelia Mambo Magumu/
Mithili ya Sumu/
Uchungu na maumivu ambayo huwezi kuvumilia/
Kaa tulia/
Futa machozi msela inatusumbua hela/
Hatuna hata kitu kidogo Cha kupeleka tumboni/
Shida zimejaa, kidogo ulichonacho, lakini bado wanatoa macho/
Lakini kwa masela, mbele kwa mbele msalie mtume/
Hapa tulipofika atakufa mtu kiume/
Kwenye Nia watabana wataachia/
Usikate tamaa mselaaaaaaa/
Vuta pumzi pumua, sononeka/
Baada ya muda utaeleweka,Usifanye haraka/
Ni kwa utulivu, na maumivu huo ndio wako mwokozi/
Piga misele mambo mazuri yapo mbele kwa mbele/
Usisikilizie viherehere/
Mbele ya hela atafia mtu jela/
Na hivi ndiyo tunavyoishi, usilete uzushi za Bob Mazishi/
Masela tuna hasira za kishashi na haziishi/
Kwani ukijituliza kimzahamzaha utakufa na ndoto kichwani/
Acha utani uwe na uchungu na thamani/
Juhudi kujitahidi ongeza bidii si kimadimadi/
Na ufike tamati,
Hakuna mipango inakamilika bila kamati/
Na bila noti, kila siku tofauti/
Usitongoze lips/
Ukiwa na matatizo Jinsi gani uta-must/
Na zitakapokutembelea namna Gani utaweka watu katikati/
Umegundua eeeeeeeeeh,
Ni yaleyale, ni kila siku baniani mbaya kiatu chake dawa/
Tafuta usawa, kidole kimoja hakivunji chawa/...

Chorus: HardMad
Mambo Mazuri yapo mbele kwa mbele/
Mbele kwa mbele/
Usikate tamaa msela ongeza misele, mbele kwa mbele/
Mambo Mazuri yapo mbele kwa mbele/
Mbele kwa mbele/
Usikate tamaa msela ongeza misele,/
Mbele kwa Mbele.

Verse 02:

Msela tulia, mambo yatatulia kama vile unalia/
Cha muhimu kuvumilia baada ya muda wenyewe watakufagilia/
Endeleza mashambulizi/
Haraka usiogope kazi, ongeza mapenzi ndani ya kazi/
Shusha pumzi,huu ndio mwisho wa majonzi/
Hakuna kipingamizi, Mungu ndiye mwamuzi/
Wewe ongeza uchungu, usikalie jungu/
Narekebisha mambo kibingwa, futa ujinga/
Tumia Kinga/
Ongeza nidhamu na uaminifu/
Umaarufu uchafu/
Wakati unatoweka ukipata nafasi ongeza Kasi/
Ondoa wasi, hakuna kitu kinapatikana kirahisi/
Nia na madhumuni ni kuleta faida na mafanikio/
Kwani masela tumeuwa kwa kipindi kirefu Sasa/
Na kazi za kueleweka wanapeana wenyewe kaka/
Kwetu sie eti hakuna elimu ya kutosha/
Wakati zingine hazihitaji kalamu Wala daftari ni kusafisha na kuosha/
Nguvu na ukakamavu unapata kiasi Cha mboga uongo/
Waziba ridhiki oooooh, wajenga chuki ooooh, wadhulumu haki oooooh wanipe Maiki oooh, niweke wazi ooohh/
Ooooh na sio ugomvi/
Ila nataka ufahamu duniani hakuna mjinga/
Kila kitu kinakuja kama sio zali basi Mungu ndivyo amepanga/
Na mbele tutasonga, kama haipo tiba basi ipo Kinga/
Sasa mbele hatusongi!!? Tunasonga...Mbeleeeeeee
 
Back
Top Bottom