Kwa wale wenzangu na mie wanandoa kuna ile hali kipindi cha uchumba na kipindi cha ndoa kabla ya kupata watoto na kuwa na wafanyakazi ndani ya nyumba kuna zile za kukumbatiana au kupigana mabusu, kulaliana kwenye makochi mkiangalia TV na vimbwanga vingine vya kimahaba vinavyofanyika nje ya chumba mfano sebuleni, jikoni na sehemu nyingine.
Je mkipata watoto inabidi vitu vile mviache na kuvifanya chumbani tu ambako kwa kawaida hamshindi huko muda mrefu au viendelee tu mbele ya watoto?
MBU umeongea point sana maana utakuta wanawake wanalalamika kuwa mbona siku hizi mapenzi yamepungua sio kama enzi za uchumba au wanamwambia mwenzake wanaume anakupenda ukiwa kwenu akikuweka ndani yale ya uchumba yote yanaisha hajui kuwa kuna vingine huwezi vifanya kukwepa watoto...No wonder wengine wakilalamikiwa "siku hizi hunijali wala hunifanyii yale ulokuwa unanifanyia zamani" wanabakia kushangaa!
Yaani usubirie mpaka mid-term au Annual leave ndio uanze 'kuibia' kwa mkeo/mumeo?
eti kwakuwa tu watoto hawapo?
aaarrggh!
hapo muwe hamna housigelo au housiboi maana nao utakuta baada ya kazi anashindilia tamthilia mpk saa sita usiku na vitoto vingine havilali mpaka viangalie kina Marichuy na Juan Miguel sasa hapo mtafanya nn zaidi ya kusubiri wakati wa kulalaJamani kwani ukikaa sebuleni baada ya msosi wa usiku, si watoto wana lala? mpigie sebuleni ili akome kulaumu kuwa humfanyii kama zamani!
Watoto wa siku hizi ukiwaacha peke yao utakuta wananyonyana ndimi, wanakumbatiana, wanafanya miujiza mikubwa usiyoitarajia.
Sijui ni wapi wanakojifunzia hizi mambo?
Mkifanya mbele yao si ndio mtakuwa unawaongezea mambinu na maujuzi?
hiyo ya kupika pamoja mie siwezi yaani katika vitu ambavyo sipendi duniani ni kupika kuna siku nilijaribu vitunguu vikaniingia machoni toka siku ile imepita miaka zaidi ya 15 sijaingia jikoni na nimeajiri house girl kumsaidia wife kwenye hiyo sector so siwezi kuingilia kabisaTV zetu zina haribu watoto wetu huu utandawazi umewatandaa vibaya.
Kuna vitu ambavyo mnaweza kuviendeleza kama kuoga pamoja, kupigana mabusu ( sio denda) mkatumia glass moja kunywea kama ni wine, juice nk wakati mnaangalia TV mkakaa kochi moja kkuangalia tv unaweza hata kumwekea mwenzi wako miguu wakati wa kuangalia TV wakati mwingine hata kupika pamoja pia mnaweza pika siku mama yuko jikoni sio vibaya baba nae akawa nae jikoni wakapika pamoja
kwa hiyo tufanye nn kimbweka tufanye mbele yao?Si wanaona kwenye Ma-TV matamthilia ya mapenzi yamejazana huko tena mida ya usiku unashangaa watoto hawaendi kulala kumbe mitamthilia ya mapenzi inasubiriwa, msipo fanya mbele yao wala haisaidii wataona huko kwenye ma-tv
kwa hiyo tufanye nn kimbweka tufanye mbele yao?
hiyo ya kupika pamoja mie siwezi yaani katika vitu ambavyo sipendi duniani ni kupika kuna siku nilijaribu vitunguu vikaniingia machoni toka siku ile imepita miaka zaidi ya 15 sijaingia jikoni na nimeajiri house girl kumsaidia wife kwenye hiyo sector so siwezi kuingilia kabisa