Mbeya: Aliyetoroka kwa kumuua mkewe anaswa na Polisi

Mbeya: Aliyetoroka kwa kumuua mkewe anaswa na Polisi

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2022
Posts
2,780
Reaction score
6,607
Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya lilifanya msako huko Kijiji cha Shitete, Kata ya Iwindi, Tarafa ya Usongwe, Wilaya na Mkoa wa Mbeya, Machi 20, 2022, ambapo walifanikiwa kumkamata SAFARI ADMIN LUWOLE [43] Mkazi wa Kijiji cha Horongo aliyekuwa akitafutwa kwa kosa la mauaji ya mke wake aitwaye TUMAINI ANTHON [45] tukio lililotokea Februari 4, 2022.

Polisi wameeleza kuwa siku ya tukio katika Kijiji cha Inolo, Kata ya Iwindi, Tarafa ya Usongwe, Wilaya na Mkoa wa Mbeya, TUMAINI Mkazi wa Inolo alikutwa ndani ya nyumba yake akiwa amefariki dunia baada ya kupigwa na kitu kizito kwenye paji la uso na mume wake, chanzo ikiwa ni ugomvi wa kifamilia kati ya marehemu na mumewe (mtuhumiwa).

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, ULRICH O. MATEI amesema Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya lilianza msako mara moja na ndipo wakafanikiwa kumkamata mtuhumiwa.

Upelelezi wa shauri hili unaendelea na mara baada ya kukamilika mtuhumiwa atafikishwa mahakamani kwa hatua zaidi za kisheria.
 
Intelijensia ya polisi inashindwaje kuzuia haya mauaji? wao wanaweza kuzuia mikutano ya CHADEMA pekee
 
Back
Top Bottom