Mbeya: Babu wa miaka 60 atupwa jela miaka 30 baada ya kukutwa na bangi

John Haramba

JF-Expert Member
Joined
Feb 4, 2022
Posts
365
Reaction score
1,374
AFUNGWA JELA MIAKA 30 KWA KOSA LA KUPATIKANA NA MICHE YA BANGI

Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya limefanikiwa kumkamata mtuhumiwa ANOSISYE AMOS MWAKITEGA [60] Mkazi wa Kyimo halmashauri ya Rungwe Mkoa wa Mbeya kwa kosa la kupatikana na miche ya bhangi 192 kinyume na kifungu cha sheria namba 11 (1) (a) cha sheria ya kudhibiti na kupambana na dawa za kulevya 2019.

Mtuhumiwa alikamatwa Machi 10, 2022 huko Kyimo halmashauri ya Wilaya ya Rungwe na kufikishwa Mahakama ya Wilaya ya Rungwe ambapo alisomewa mashitaka matatu:

1. Kulima miche ya bhangi 192 kinyume na kifungu namba 11 (1) (a) cha sheria ya kudhibiti na kupambana na dawa za kelevya ya mwaka 2019
2. Kupatikana na bhangi gramu 410
3. Kupatikana na bhangi gramu 12.3 kinyume na kifungu namba 17 (1) (a) na (b) ya mwaka 2019 iliyofanyiwa marejeo mwaka 2021.

Mnamo Machi 15, 2022 mtuhumiwa alipatikana na hatia kwa makosa yote matatu na kuhukumiwa kifungo jela miaka thelathini [30].

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi, ULRICH MATEI anatoa rai kwa wananchi kuacha kujihusisha na biashara ya dawa za kulevya na badala yake watafute shughuli nyingine halali zitakazowapatia kipato halali.

Aidha, Kamanda MATEI anawataka wananchi kuacha mara moja matumizi ya dawa za kulevya kwani ni kinyume cha sheria n ani hatari kwa afya zao na watakapokamatwa na kufikishwa mahakamani watafungwa.
 
yaani wamemkamata tarehe 10 na tarehe 15 amekutwa na hatia amehukumiwa kwa kosa la kukutwa na mimie aliyoiumba Mungu, huu ni upuuzi kabisa, wamuachie huyo mzee, bangi sio haramu kuilima, kumiliki wala kuitumia, maelfu ya watanzania wanakufa kwa uvutaji wa sigara kila mwaka liakini ipo na inaendelea kuuzwa, serikali ituambie kila mwaka ni watu wangapi wanakufa kwa matumizi ya bangi?
 
Kweli maskini haki yake iko Mbinguni. Siyo kwa uonevu huu. Maana bangi ilikuwepo, ipo na itakuwepo! Na watu walivuta bangi, wanaendelea kuvuta, na watavuta mpaka siku ya mwisho!

Hivyo binafsi naona huyo mzee kaonewa tu. Angekuwa amebaka mjukuu wake, ningeunga mkono hiyo adhabu! Ila siyo kwa kosa la bangi ambayo imetapakaa mtaani! Huku baadhi ya hao polisi na mahakimu na wenyewe wakipuliza 🚬 vizuri tu.
 
Mikoa ya nyanda za juu kusini wanaiogopa Bangi kuliko ngwengwe. Iringa, Njombe hadi Mbeya wakuone tu umeweka hata fegi mdomoni.

Huyo mzee angekuwa wa Moro, Mara, au Arusha sasa hivi angekuwa katulia uraini
 
Na kuna sehemu wanaitumia Kama Mboga. Hivi ule mjadala wa kuhalalisha Bangi kwa baadhi ya matumizi, ikiwemo Kuwa kama Dawa haukukamilisha mchakato?
 
AFUNGWA JELA MIAKA 30 KWA KOSA LA KUPATIKANA NA MICHE YA BANGI

Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya limefanikiwa kumkamata mtuhumiwa ANOSISYE AMOS MWAKITEGA [60] Mkazi wa Kyimo halmashauri ya Rungwe Mkoa wa Mbeya kwa kosa la kupatikana na miche ya bhangi 192 kinyume na kifungu cha sheria namba 11 (1) (a) cha sheria ya kudhibiti na kupambana na dawa za kulevya 2019.

Mtuhumiwa alikamatwa Machi 10, 2022 huko Kyimo halmashauri ya Wilaya ya Rungwe na kufikishwa Mahakama ya Wilaya ya Rungwe ambapo alisomewa mashitaka matatu:

1. Kulima miche ya bhangi 192 kinyume na kifungu namba 11 (1) (a) cha sheria ya kudhibiti na kupambana na dawa za kelevya ya mwaka 2019
2. Kupatikana na bhangi gramu 410
3. Kupatikana na bhangi gramu 12.3 kinyume na kifungu namba 17 (1) (a) na (b) ya mwaka 2019 iliyofanyiwa marejeo mwaka 2021.

Mnamo Machi 15, 2022 mtuhumiwa alipatikana na hatia kwa makosa yote matatu na kuhukumiwa kifungo jela miaka thelathini [30].

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi, ULRICH MATEI anatoa rai kwa wananchi kuacha kujihusisha na biashara ya dawa za kulevya na badala yake watafute shughuli nyingine halali zitakazowapatia kipato halali.

Aidha, Kamanda MATEI anawataka wananchi kuacha mara moja matumizi ya dawa za kulevya kwani ni kinyume cha sheria n ani hatari kwa afya zao na watakapokamatwa na kufikishwa mahakamani watafungwa.
Mambo ya kijinga,haitakiwi kabisa kuendeyna sheria za kipuuzi kama hizi.
 
Kweli maskini haki yake iko Mbinguni. Siyo kwa uonevu huu. Maana bangi ilikuwepo, ipo na itakuwepo! Na watu walivuta bangi, wanaendelea kuvuta, na watavuta mpaka siku ya mwisho!

Hivyo binafsi naona huyo mzee kaonewa tu. Angekuwa amebaka mjukuu wake, ningeunga mkono hiyo adhabu! Ila siyo kwa kosa la bangi ambayo imetapakaa mtaani! Huku baadhi ya hao polisi na mahakimu na wenyewe wakipuliza 🚬 vizuri tu.
Kama masikini wataingia Jehanam wa appeal kwa Sir God.
 
Mikoa ya nyanda za juu kusini wanaiogopa Bangi kuliko ngwengwe. Iringa, Njombe hadi Mbeya wakuone tu umeweka hata fegi mdomoni.

Huyo mzee angekuwa wa Moro, Mara, au Arusha sasa hivi angekuwa katulia uraini
Kuhusu Moro umenigusa nadhani Yale nimashamba ya serikali Mana sikwa ule ukubwa mwananchi ukiwa mgeni maeneo Yale saa 8 uck usiamke kukojoa nje labda wawe wamekufahamu huna madhara
 
Moro pande zipi?
Sema waluguru wangese sana, wakimshtukia mnoko wanamzima na kuzika ushahidi.
 
Back
Top Bottom