Mwanongwa
JF-Expert Member
- Feb 15, 2023
- 611
- 567
Wakazi wa mtaa wa Ntundu kata ya Nsalaga jijini Mbeya wameingiwa na mchecheto baada ya taarifa ya fedha ya balozi wao Laulian Kiyeyeu kuwa na ukakasi.
Tukio hilo lilijili mnamo tarehe 6 ya mwezi huu wa nne kwenye mkutano wa ubalozi ambao huwa unafanyika kila tarehe sita ya kila mwezi.
Mwanzoni kulikuwa na tetesi za kuwa balozi huyo ambaye hivi karibuni alikumbwa na kashfa ya upigaji wa fedha za umeme wa Rea,kuwa amepiga tena fedha ya ubalozi.
Wakizungumza wananchi wamesema kuwa kuna kiasi cha shilingi laki tatu ambacho hakijulikani kiliko.
Wananchi hao walipombana sana balozi kwenye mkutano huo,akawaambia kuwa fedha hizo amemkabidhi mdau mmoja wa maendeleo anayejulikana kwa jina la Mwezi Mpya.
Lakini baada ya baadhi ya wananchi kumtafuta Mwenzi mpya na kumuuliza alisema kuwa hakuna fedha yoyote ambayo amekabidhiwa na kiongozi huyo huku akisema kitendo hicho siyo cha kiungwana na kinamchafua mbele ya jamii.
"Hakuna pesa yoyote ambayo huyo balozi kaileta kwangu na kitendo cha kusema kuwa amenipa Mimi kinanichafua mbele ya jamii maana watu wanaweza kuhisi kuwa nashirikiana naye kwenye uhujumu huo".
Wananchi wa mtaa huo wa Ntundu wamempa muda wa wiki moja balozi huyo awe amekabidhi pesa hizo kwa mtunza hazina na zipelekwe Benki.