LGE2024 Mbeya: CCM Kata ya Ibililo Kijiji cha Nkunga kimenuka

LGE2024 Mbeya: CCM Kata ya Ibililo Kijiji cha Nkunga kimenuka

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024

Mwanongwa

JF-Expert Member
Joined
Feb 15, 2023
Posts
611
Reaction score
567
Kuelekea uchaguzi wa Serikali za Mitaa sasa kumeanza kuchanganya sana.

Vuta ni kuvute imetokea ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika Kata ya Ibililo Kijiji Cha Nkunga Wilayani Rungwe.

Picha linaanza kamati ya siasa imepitisha jina ambalo wajumbe wamelichagua lakini Katibu wa Chama kapeleka jina lingine Wilayani.

Wanachama wamechachamaa wanadai wako tayari kuwapa kura chama pinzani kutokana na jambo hilo

Uchaguzi wa safari hii umekuwa na pilika pilika sana ndani ya chama tawala hata vyama vya upinzani.

Wananchi tujitokeze Kwa wingi kuchagua viongozi ambao tunawataka watuongoze kwa miaka mitano ijayo.
 
Back
Top Bottom