Mwanongwa
JF-Expert Member
- Feb 15, 2023
- 611
- 567
Hili Jiji la Mbeya licha ya kukumbwa na ugonjwa wa Kipindupindu ambao kila siku tunasikia Serikali inapambana nao lakini hali ya uchafu katika baadhi ya maeneo inaendelea kuongezeka.
Na hizi mvua zinazoendelea kunyesha ndiyo zinazidi kusambaza uchafu mitaani. Leo katika pitapita zangu nikajikuta nimeibukia Mitaa ya Forest ya Zamani karibu na Shule ya St. Francis Girls.
Katika mtaa huo kuna chemba mbili za maji taka zinavuja vibaya mno na maji yote machafu yanaelekea Barabarani.
Soma pia: Takataka zimekuwa kero kubwa sana Mbeya Mjini kipindi hiki cha mvua
Kibaya zaidi yanatoa harufu kali sana na pembeni yake Kuna Hoteli ya FQ na hiyo Shule niliyoitaja ya St.Francis.
Hii imekuwa ni kero kubwa sana lakini wahusika ambao ni Idara ya Maji Mkoa wa Mbeya wako kimya tu kama hawaoni, watu wengine wanapita wanaona maji machafu yenye kinyesi yanasambaa mitaani wanachukulia poa tu, kwa msingi huu, Kipindupindu kitaisha kweli?
Kwa mwenendo huu ni ngumu sana magonjwa ya mlipuko kuisha.