Mbeya city & Ihefu zashinda PLAY OFF

AirSongwe

Member
Joined
Jun 13, 2019
Posts
72
Reaction score
90
Hongera Ihefu kupanda ligi kuu Kwa kumtoa Mbao kwenye play off Kwa faida ya goli la ugenini na Mbeya city kumtoa Geita FC.
Mkoa wa Mbeya Sasa timu 3 msimu ujao.
 
Nawaomba Tanzania Prisons ihamie Rukwa, itapiga hela sana maana nimefatilia kwenye media nimeona walivyoamsha popo kuhusu fainali ya SIMBA NA NAMUNGO
 
Hizi play off za bongo ni za kipuuzi sana. Ni dhahiri zimeundwa na watu wasio na utashi toshelezi. Ni upuuzi kutengeneza uwezekano wa timu iliyoshindwa kupigania nafasi yake msimu mzima kusalia kwenye ligi kwa kuifunga timu iliyopigania kupanda msimu mzima.

Play off zapaswa kukutanisha timu zilizokuwa zikipigania kupanda daraja. Tena nafasi ya play off yapaswa kuwa moja tu, ipiganiwe na timu 4 au 6 yaani kuanzia nafasi ya 3 mpaka 6 au 8 kwenye msimamo.
 
Tumelichukua wazo, lakini sio mbaya hizi zinazopanda tukazipima na hizi za ligi kuu ili kulinda ubora.

Wakizitoa kweli tutajua wao wa daraja la kwanza wamekomaa kucheza ligi kuu.
 
zipo zinazopanda direct na zinazoshuka direct, then nafasi mbili za ziada ndio playoff.......


kumbuka tpl zimeshuka timu 4 direct, lipuli, ndanda, singida na alliance, na zimepanda mbili direct (nadhani),
 
Tumelichukua wazo, lakini sio mbaya hizi zinazopanda tukazipima na hizi za ligi kuu ili kulinda ubora.

Wakizitoa kweli tutajua wao wa daraja la kwanza wamekomaa kucheza ligi kuu.
Naamini kipimo cha mechi mbili au nne si cha haki kabisa. Kipimo cha haki ni kile cha kucheza mechi zaidi ya 20 au 30 msimu mzima. Ikumbukwe kuwa timu iwe kubwa au ndogo hupitia vipindi tofauti ndani ya msimu mzima. Hivyo kipimo kizuri zaidi ni kile kinaochojumuisha mkusanyiko wa pointi angalau kwa kipindi kirefu (msimu).

Case 1: Timu ya daraja la kwanza inaweza kuwa ilipambana msimu mzima ikawa ya pili ila ikacheza play off kwenye kipindi ambacho haiko kwenye form.

Case 2: Timu ya ligi kuu inaweza kupuyanga msimu mzima na ikawa haina tena sifa za kubaki ligi kuu. Lakini kwa kuwa huwa na kikosi na benchi na mashabiki komavu na zoefu inaweza kujipanga vema kwa ajili ya fixture moja tu ya play off. Hapa uzoefu ni dawa hata kama timu ni dhaifu.

Mfano mzuri hapa ni Mbeya City. Ndiyo ni timu yangu ila usishangae ikarejea msimu ujao na kupokea vipigo mfululizo kama ilivyokuwa msimu huu ulioisha.

Ukitaka kuelewa zaidi rejea ubora wa Liverpool kwa sehemu kubwa ya msimu huu kabla ya kipigo cha Watford. Sasa jaribu kujenga picha kuwa ile ndiyo ingekuwa ni fixture ya kuhusu kushuka au kupanda daraja! Timu iliyosimama imara kwenye mabonde na milima kwa karibu msimu mzima inapoteza fixture kwa timu iliyodorora.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…