Mbeya City Vs Simba Sports Club: Mbeya City yalala nyumbani kwa goli moja dhidi ya Simba

Ghazwat

JF-Expert Member
Joined
Oct 4, 2015
Posts
23,718
Reaction score
66,267
VPL.. Ni kama vile jiji la Mbeya limesimama kwa muda na gumzo kubwa ni mbungi itakakayopigwa leo katika uwanja wa CCM Kumbukumbu ya Sokoine kati ya Mbeya City, na Mnyama Simba Sports.

Muda huu wa saa 6.20 mchana, watu wanazidi kumiminika uwanjani huku foleni za kukata tiketi zikiongezeka kama inavyoonekana hapa.

Kumbuka mechi hii itakuwa mubashara kupitia Azam Sports 2 na kwa upande wa radio TBC Taifa inakutangazia kuanzia saa 10. 00 jioni.

Vikosi vyote viwili tukianza na wenyeji wa mchezo huu, Mbeya City:

Upande wa wageni wa mchezo huu, Simba Sports Club:

=======

Timu ndo zinaingia uwanjani kuashiria kuanza kwa mpambano

==> 0' Mpira umeanza: Mbeya City 0-0 Simba Sports Club

==> Goooooaaal dakika ya 8' Shiza Kichuya anaipatia Simba SC goli la kwanza, Mbeya City 0-1 Simba SC

==> 15' Mbeya City 0-1 Simba SC

==> 30' Mbeya City 0-1 Simba SC

45 ' za kipindi cha kwanza za mchezo wa mpira zimekwisha ambapo matokeo ni Mbeya City 0-1 Simba Sports Club.

Half time;

45' za kwanza kipindi cha pili za mtanange huu zinaanza

==> 65' matokeo bado Mbeya City 0-1 Simba Sports Club

==> 80' Mbeya City 0-1 Simba Sports Club

90+3' Mpira umekwisha kwenye uwanja wa Sokoine, Mbeya City ikiwa nyumbani imefungwa goli moja bila majibu, goli likifungwa na winga Shiza Kichuya akipokea pasi safi kutoka Jonas Mkude.

Kwa matokeo hayo Simba SC imerejea kileleni mwa msimamo wa ligi kuu Tanzania bara (VPL), kwa alama 19 huku Ruvu Shooting ikisalia mkiani na alama zake 5.
 
1' Mbeya City watapata kona hapa ambayo haijazaa matunda mpira umeanza kwa kasi
 
[emoji122][emoji122][emoji122][emoji122][emoji122][emoji119][emoji119]
 
Go gooal hapana, John Bocco anakosa goal la wazi hapa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…