Pole sana. Mimi nilikuwa na kawaida ya kufikia hapo. Kuna siku nikaenda hapo kama saa 12 hivi nikitokea Dar Kwa Sumry nikaambiwa mmiliki wake alipata ajali na kufariki siku hiyo saa 9.00 Mchana. Hivyo nikaenda kukaa ktk hotel inaitwa Paradise bahati mbaya nilikuwa nimepoteza kadi ya Benki hivyo nilikuwa na fedha taslimu kwa ajili ya Semina. Nilikuwa natoka nazo siku zote (mbili)zikiwa kwenye mfuko wa laptop hadi nikalipa na kubakiwa na Tsh 1,500,000/= basi kukawa na onyesho la Makhirikiri karibu na hapo nikaenda na kufanya kosa la kuacha zile fedha kwenye Begi (wanaziita Pilot Bag)
Nilivyorudi kitu cha kwanza nikaangalia nikakuta pesa iko nikalala na hiyo begi haijafunguliwa iko kama nilivyoiacha. Kuamka asubuhi nikalipe nikakuta kila fungu la laki moja inapungua elfu 30,000/=. Nikafanya uhakiki nikakuta kumbe nililizwa pia soksi mpya kama pea mbili, na underwear mpya kama mbili hivi. Hapo ndipo nilipowaaminia.
Nikashuka chini kuripoti nikakutana na bango kuwa vitu vyote vya thamani ikiwa ni pamoja na PESA vikabidhiwe mapokezi!! Upotevu wowote Hoteli haitasikiliza hata kidogo.
Hivyo nikaghairi kuripoti hilo tukio.
Hata hivyo ni hatari sana kukabidhi fedha kiasi kikubwa kwani kuna jamaa yangu alifanya hivyo siku anaondoka akakutana na vijana wenye piki piki pale tu nje ( Siyo Paradise) wakimtaka awakabidhi haraka kiasi hicho bila kuchelewa kwani walikuwa wanawahi kumwua jamaa mwingine hapo mbele
Hivyo wizi upo sehemu nyingi cha kufanya ni kuchukua tahadhari ya hali ya juu, ikiwa ni pamoja na kutokabidhi pesa kaunta.