The Watchman
JF-Expert Member
- Nov 7, 2023
- 896
- 1,427
Hapa ni kitongoji cha Hasengo, kijiji cha Shibolya wilaya ya Mbeya vijijini mkoani Mbeya, Ni jambo jema na tunashukuru huduma ya umeme imetufikia kupitia wakala wa kusambaza umeme vijijini REA, baada ya kutokuwepo kwa huduma hiyo muhimu tangu kupata uhuru wa nchi hii.
Bila shaka usambazaji wa huduma hii kwa wananchi unapaswa pia kuzingatia usalama wa watu kutokana na hatari kubwa ya umeme. Kilichofanyika hapa kwetu ni kuhatarisha maisha ya watu hasa watoto wadogo. Ufungaji wa namna hii wa nyaya za umeme kama kamba za kuanikia nguo ni hatari sanaa,
Na bado hapo katikati waya unabembea karibu mtu yeyote anayepita hapo anaweza kuufikia na kushika na watoto pia hucheza karibu na hapo, hii ni hatari zaidi
Nyaya zinatepeta ni kwamba TANESCO & REA mmeishiwa nguzo mpaka mnafunga nyaya za umeme kama kamba za kuanikia nguo?
TANESCO pamoja na REA mfanyie kazi changamoto hii ili kuweka maisha ya watu salama kwa kuondoa hatari hii