Mbeya: Jeshi la Polisi lamkamata wakala wa bima ya GTM baada ya kukumta mihuri 56 ya kughushi ya idara za serikali na ofisi binafsi

Mbeya: Jeshi la Polisi lamkamata wakala wa bima ya GTM baada ya kukumta mihuri 56 ya kughushi ya idara za serikali na ofisi binafsi

Suley2019

JF-Expert Member
Joined
Oct 7, 2019
Posts
2,203
Reaction score
5,610
Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linamshikilia ABRAHAM OBEDI [55] wakala wa bima ya GTM na Mkazi wa Isanga Jijini Mbeya akiwa na mihuri hamsini na sita [56] ya idara mbalimbali za serikali na ofisi binafsi ambayo imeghushiwa na kuhifadhiwa katika ofisi yake ya Stationaries.

Mtuhumiwa alikamatwa Disemba 31, 2019 majira ya saa 17:00 jioni huko maeneo ya Mtaa wa Sokoine uliopo Kata na Tarafa ya Sisimba Jijini Mbeya baada ya Jeshi la Polisi Mkoani hapa kupata taarifa na kisha kufanya msako mkali na kufanikiwa kumtia nguvuni mtuhumiwa pamoja na vielelezo.

Baadhi ya mihuri na nyaraka alizokutwa nazo mtuhumiwa ni kama ifuatavyo:-

1.Mhuri wa Mwenyekiti wa Mtaa wa Soko Kata ya Ruanda,

2.Mhuri wa Afisa biashara wa Halmashauri ya Mbeya,

3. Access Bank Tawi la Mbeya,

4.Mamlaka ya Mapato Mbeya [TRA]

5. Hakimu Mkazi Mahakama ya Mwanzo Mbeya Mjini,

Aidha mtuhumiwa alikutwa pia na Kompyuta moja aina ya Accer, Stika za bima, Poss Machine na nyaraka mbalimbali vikiwemo vyeti vya wanafunzi ambao vimeghushiwa. Upelelezi wa shauri hili unaendelea na mara baada ya kukamilika mtuhumiwa atafikishwa mahakamani kwa hatua zaidi za kisheria.

KUPATIKANA NA BANGI.

Jeshi la Polisi Mkoani hapa linamshikilia AGREY MASHAKA MBOTO [25] Mkazi wa Kilambo Wilayani Kyela akiwa na dawa za kulevya aina ya bangi kavu kilogramu thelathini [30].

Mtuhumiwa alikamatwa Disemba 31, 2019 majira ya saa 14:45 mchana baada ya Jeshi la Polisi Mkoani hapa kufanya msako mkali huko Kitongoji cha Kilambo, Kata ya Njisi, Tarafa ya Unyakyusa, Wilaya ya Kyela na Mkoa wa Mbeya. Mtuhumiwa ni muuzaji na mtumiaji wa bangi hiyo.


Malunde blog
 
Huu ndio uanaume Sasa, jamaa angetenegeneza na muhuri wa dokta wa vichaa ili mahakama imwachie huru.

Fake it untill you make it! [emoji38]


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huyo ni mchonga mihuri hivyo ile inayoharibika hubaki nayo ndo anakuja kuirekebisha na kufanyia uhalifu kwa njia ya uaminifu
 
Back
Top Bottom