KERO Mbeya jiji: Kuna Watu wanaotishia waendesha bajaji, hawafanywi chochote na yeyote eneo la geti la Pili kwenye bandari kavu

KERO Mbeya jiji: Kuna Watu wanaotishia waendesha bajaji, hawafanywi chochote na yeyote eneo la geti la Pili kwenye bandari kavu

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua

gcmmedia

Member
Joined
Jul 19, 2024
Posts
34
Reaction score
75
Kuna kundi la watu wapo eneo la Geti la Pili kwenye bandari kavu jijini Mbeya, mbele kidogo ya Iyunga unapoelekea Mbalizi. Watu hawa hukamata bajaji mchana kweupe wakiwa na marungu kuzuia bajaji zisiende uelekeo wa Mbalizi.

Cha kushangaza, hata kama umekodi bajaji hawa watu hawataki hilo. Wanawasumbua mkodishaji na dreva wa bajaji; hadi wapewe pesa na dreva bajaji ndiyo huwaachia kuendelea. Wana kiburi sana.

Swali ni, Je, watu hawa ni mamlaka gani? Nani kawapa mamlaka hii kubwa? Kwa nini mamlaka husika zipo kimya? Nani yupo nyuma yao?
 
Hao ni wamiliki wa costa ziendazo Mbalizi wanahisi mnaelekea kuharibu biashara yao kama mlivyoharibu daladala za Kabwe to Iyunga
 
Hao ni wamiliki wa costa ziendazo Mbalizi wanahisi mnaelekea kuharibu biashara yao kama mlivyoharibu daladala za Kabwe to Iyunga
Aah, kumbe! Kwa hiyo wanaruhusiwa kufanya hivyo?
 
Back
Top Bottom