Dong Jin
JF-Expert Member
- Jun 4, 2018
- 968
- 2,034
Mchakato wa kuwapata waandishi wa daftari la kudumu kwa Mbeya mjini ni wa hovyo kuliko kawaida. Hii ni rushwa ya waziwazi inafanyika.
Watu waliomba ajira na waliopita wapo. Kwanini msitoe majina na kuyabandika katika mbao za matangazo au tuyaone kwenye tovuti yenu km walivyofanya maeneo mengine badala yake mmekuwa mkiwapigia simu waliopata na kuwaambia waende ijumaa (ambayo ni kesho) kwenye interview.
Sasa ni kwanini muwapigie simu na msitoe majina? Kama sio rushwa ni nini? Kulikuwa kuna haja gani ya kuwasumbua watu watume maombi?
Huu ni upuuzi na mnauendesha mchakato kwa rushwa na kujuana. Sitashangaa kuona watu ambao hawakuomba kabisa nikawakuta hiyo kesho hapo mbeya secondari wamekuja kwenye interview.
Mamlaka ya kupambana na kuzuia rushwa jaribuni kulichunguza suala hili ili kila anayestahili apate haki yake