Mbeya: Kata ya Serengeti mabingwa wa Mashindano ya Kyela Polisi Jamii Cup 2023

Mbeya: Kata ya Serengeti mabingwa wa Mashindano ya Kyela Polisi Jamii Cup 2023

BigTall

JF-Expert Member
Joined
Mar 9, 2022
Posts
525
Reaction score
1,257
Mkuu wa Wilaya ya Kyela, Josephine Manase Keenja, Mei 01, 2023 amefunga rasmi mashindano ya mpira wa miguu yajulikanayo kwa jina la "KYELA POLISI JAMII CUP, 2023" baada ya kushuhudia fainali iliyozikutanisha timu za Kata ya Ipinda dhidi ya Kata ya Serengeti.

1.jpg
Mashindano hayo yalihusisha Kata 33 za Wilaya ya Kyela na hatua ya robo fainali ziliingia Kata nane huku hatua ya nusu fainali ziliingia Kata nne na fainali ziliingia Kata mbili ambapo Kata ya SERENGETI imeibuka mshindi wa mashindano hayo baada ya kupata ushindi wa magoli 2 kwa bila dhidi ya Kata ya Ipinda.

Akizungumza wakati wa kufunga mashindano hayo, Mkuu wa Wilaya ya Kyela Mhe.MANASE amelipongeza Jeshi la Polisi kwa kuandaa mashindano hayo yenye lengo la kuiweka jamii karibu na Jeshi la Polisi na kuweza kupata taarifa mbalimbali za kihalifu na wahalifu.

2.jpg
Pia, kupitia mashindano hayo jamii imepata elimu kwa urahisi hasa ya kupinga ukatili wa kijinsia na unyanyasaji dhidi ya wanawake na watoto.

Masane ameongeza kuwa, kupitia mashindano hayo, vijana wamepata ajira kupitia michezo pamoja na kuibua vipaji vyao hali inayowafanya kujiepusha na vitendo vya kihalifu.

3.jpg

Mbeya Polisi 2.jpg

Naye, Mkuu wa Polisi Wilaya ya Kyeya SSP Lwitiko Kibanda ameeleza matarajio ya Jeshi la Polisi baada ya kumalizika kwa mashindano hayo kuwa ni, kupata taarifa za wahalifu kabla ya kutenda uhalifu, kupunguza na kukomesha matukio ya ukatili wa kijinsia kupitia elimu iliyotolewa, kuiweka jamii karibu na Jeshi la Polisi na kuongeza ajira kwa vijana kupitia michezo.

4.jpg
Zawadi zilizotolewa kwa bingwa ni N'gombe dume mmoja, Mbuzi na jezi pea moja kwa shindi wa pili, Mpira mmoja mpya kwa mshindi wa tatu, Mshindi wa 4 hadi wa 33 ni huduma zote za uwanjani.

Mashindano ya "Kyela Polisi Jamii Cup, 2023" yalifunguliwa rasmi na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya ACP Benjamin Kuzaga Aprili 19, 2023.

Mbeya Polisi.jpg
 
Haya mashindano mahali kwingine yana ujanjaujanja sana
 
Back
Top Bottom