Mbeya: Mbunge Masache Kasaka afika Kata ya Ifumbo, Lupa Wilayani Chunya

Mbeya: Mbunge Masache Kasaka afika Kata ya Ifumbo, Lupa Wilayani Chunya

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2020
Posts
2,833
Reaction score
1,301

MBUNGE KASAKA APOKELEWA KWA KISHINDO IFUMBO

Mbunge wa Jimbo la Lupa Masache Njelu Kasaka amemalizia ziara yake ya Kata kwa Kata na amewafikia wana Ifumbo na kutembelea Vijiji viwili vya Lupa Market pamoja na Ifumbo.

Katika ziara yake Mhe. Mbunge ameongea na wananchi na kuwapa mrejesho wa Utekelezaji wa Ilani ya CCM ambapo Kata ya Ifumbo imeweza kufaidika katika sekta ya miundombinu ya Barabara, Upatikanaji wa maji, pamoja na ujenzi wa zahanati na uboreshwaji wa zahanati ya Ifumbo.

Mhe. Kasaka pia amesikia changamoto za wana Ifumbo ambapo kilio chao kikubwa ni kusimamishwa kwa mwekezaji raia wa China, kuacha shughuli za uchimbaji pembezoni mwa mto Zilla.

Mhe. Kasaka amelipokea na ameahidi kulifikisha kwa mamlaka husika ili wana Ifumbo waweze pata suluhisho la kudumu kwa jambo hilo.

F8LnYZ-XAAAXIOp.jpg
F8LnY9PXsAAIROS.jpg
F8LnZZFWcAArt4g.jpg
 
Back
Top Bottom