Mkalukungone mwamba
JF-Expert Member
- Aug 29, 2022
- 862
- 1,755
Mkuu wa mkoa wa Mbeya Mhe. Juma Homera ameelekeza uongozi wa jiji la Mbeya, kusitisha mkataba wa mkandarasi anayejenga vyumba vitatu vya madarasa na vyoo, katika shule ya msingi mafanikio kata ya Itezi jijini Mbeya kwa kushindwa kukamilisha madarasa hayo kwa wakati.
Madarasa hayo yanayojengwa kwa fedha kutoka serikali kuu kiasi cha shilingi millioni 88, fedha zilizo tolewa mwezi wa sita mwaka 2024, lakini ujenzi wake umekua ukisuasua hadi sasa ukiwa bado haujakamilika, huku mkandarasi akiwatishia wananchi wa eneo hilo kua ni mjumbe wa kamati ya nidhamu wa chama cha mapinduzi CCM, ili kuwazuia kumfuatilia kwa ukaribu.
Nao baadhi ya mafundi waliotumiwa na mkandarasi kutekeleza mradi huo wameeleza namna mkandarasi huyo alivyofanya dhuluma kwao kwa kuwapa kazi bila malipo ambayo wanadai hadi sasa, huku mstahiki Meya wa Jiji la Mbeya Mhe. DorMohamed Issa akieleza maamuzi yaliyofikiwa na uongozi wa jiji hilo.