Habari wanajukwaa!
Je, kuna utaratibu wowote kwa shule ya Sekondari kuamuru kumfukuza shule mtoto mwenye ufaulu hafifu?
Nimekutana na hii scenario katika shule moja ya Sekondari iliyopo mtaa wa Mabatini, Kata ya Mabatini, Wilaya ya Mbeya Jiji, Mkoa wa Mbeya. Hii shule inaitwa Mabatini Secondary School, wiki hii mwalimu mkuu wa shule ameita wazazi shuleni kwa ajili ya kutoa taarifa.
Taarifa iliyotolewa ni kwamba kwa baadhi ya wanafunzi ambao wana ufaulu hafifu hasa hawa wa kidato cha pili ambao mwaka jana walikuwa kidato cha kwanza wanatakiwa kurudia darasa na kama ikitokea wamegoma waachane na shule na kujiunga na mafunzo ya Ufundi ambayo yametolewa na Serikali hivi karibuni.
Naulizia kupata muongozo, je, hii inakubalika?
Akielezea kuhusu suala hilo, Mkurugenzi wa Mbeya Jiji, John John Nchimbi amezungumza na JamiiForums na kusema:
“Suala hilo halijafika kwangu lakini nimekuwa mara zote nikiwashauri Wazazi au Walezi wenye malalamika au wanahisi wameonewa wasiishie kuandika Mtandaoni, waje ofisini kwangu tuzungumze.
“Mtoto hawezi na haitakiwi kurudishwa darasa bila mzazi kujua au kwa lazima, ikitokea kuwa hakuwepo darasani muda mrefu hapo anaweza kurudishwa lakini kwa Mzazi kupewa taarifa ya maandishi.
“Nawakaribisha wote wenye changamoto, wiki hii nipo ofisini, waje kuanzia saa mbili asubuhi watanikuta, nipo kwa ajili yao."
Afisa Elimu Mkoa wa Mbeya, Mwalimu Kiduma Mageni alipozungumza na JamiiForums amesema:
"Kama Mwalimu anafanya hivyo anakosea na nikinyume cha utaratibu, Mwanafunzi kurudia inatakiwa ridhaa ya Mzazi na baada ya mazungumzo inatakiwa athibitishe kwa maandishi, pia mimi ndio ninayepitisha huo uamuzi wa Mwanafunzi kurudia darasa, hivyo suala hilo nitalifuatilia kwa ukaribu."

=========================
Mkurugenzi wa Jiji: Wazazi wenye malalamiko wafike ofisini kwangu