Uchaguzi 2020 Mbeya na Iringa bado ngoma ngumu kwa CCM

MJITAHIDI KUTUNZA HIZI THREAD ZENU MAANA BAADA YA OCTOBER 30 SIAMINI KAMA MTAKUWA NA UWEZO WA KUCHANGIA MADA KWA JINSI MTAVYOKUWA MMELOWA JASHO LA KUSHINDWA
 
Katika majimbo yote ya upinzani jimbo ambalo labda Chadema wanaweza kupoteza ni Kibamba.

Lakini nayaona majimbo mengine ya wazi yakiangukia Chadema tena asubuhi tu mfano Kyela, Mbarali, Mafinga mjini, Mororgoro mjini, Ilala. Pia majimbo ambayo CCM watashinda basi kutakuwa na uwiano mdogo sana wa kura. Kiukweli nimewasifu watanzania sasa wanaiona siasa kama kazi isiyohitaji masihara!

Kitu kingine Magufuli ana uwanja mdogo sana wa kujinadi ambao ni miundombinu na hilo kila kiongozi analiweza. Magufuli pia hataweza kujinadi kwa hilo maana amekuwa akilizungumza kwa miaka yote mitano! Hawezi kuwaambia watu eti ataajiri au kuongeza mshahara wamuelewe maana tayari alishawadanganya 2015 baada ya kushindwa kutekeleza mengi.

Kiukweli Lissu ana uwanja mpana na atakapokuwa anahutubia kwanza wananchi watakuwa na kumbukumbu ya yeye kupigwa risasi, uminywaji mkubwa wa haki na mengine mengi. Magufuli atakuwa hadi anaona aibu mbele za watu hasa kwa swala la mpinzani wake kupigwa risasi na hajafanya kitu kama kiongozi.

Kitu kingine Magufuli hachelewi kuharibu wakati wa kuhutubia maana wameshaona kila hotuba. Kumbuka kuwa kipindi hiki ana kiburi na amekionyesha waziwazi kwa watanzania. Kitu ambacho ni tofauti kabisa na alipokuwa akihutubia mwaka 2015! Alikuwa anaonyesha upole na unyenyekevu mkubwa.

Kuna maeneo akienda kwanza itamlazimu aanze kuweka hali sawa kama Kusini, Kagera na Kaskazini. Kumbuka kuwa Magufuli Kaskazini hajawahi kufanya ziara ya kimaendeleo na hajapeleka chochote kile zaidi ya hilo treni ambalo kimsingi kwa watu wa Kaskazini ni useless! Magufuli alikosea sana kujitenga na kuikumbatia njia yake ya uelekeo wa Chato! Halafu dhambi ya ubaguzi ameionyesha wazawazi!

Halafu ndani ya CCM kwenyewe mfano mtu kama JK hata anavyoongea unaona kabisa hamkubali hata kidogo Magufuli. Mwisho wa yote mtu ambaye walimtegemea kuwa anaweza kuongea kitu kikaingia masikioni na alikuwa mtetezi mkubwa wa kutegemewa wa Magufuli ameshaaga dunia! Aliyebaki Mwinyi hana point, JK ndo hivyo akiongea hadi kina Hapi kule Iringa wanarusha mawe!

Mwisho kabisa tegemeeni kusikia mtu au watu ndani ya CCM wakiropoka kuhusu matukio ya watu kupotea, Lissu kupigwa risasi na mengine mengi. Kiuhalisia Magufuli amejijengea taswira mbaya sana ya ubinadamu machoni pa watanzania kitu ambacho watanzania wengi wanakithamini kwa nguvu kubwa!
 


Best Morogoro mjini itoe hapo umejimix
 
Akipiga Kura kila kitu akachukue ofisi za CCM asitegemee kitu au support yyt kutoka kwangu! Yaani namaanisha!


Usifanye hivyo,
kipimo umpimiacho mtu ndicho utakachopimiwa.

Kwa vile sio kosa kisheria kuwa na tofauti za kimtazamo, usimfanyie hivyo. Kama ameshindwa kukuelewa achana naye
 
Chadema wakiungana na ACT watapata viti vya ubunge 60 percent na Urais Lissu anashinnda kwa 70 percent ili halina mjadala.
LISU hapati zaidi ya 20%

Hili suala watu wanaona kama napiga propaganda ila ndio ukweli
 
Nadhani ni wkt wa Pascal Mayala kujifunza kutoka kwenye huu uchambuzi..asiegemee upande wwte

Kaka Pascal alitegemea hisani kwenye uchaguzi huu. Huoni aligombea?

Ukishakuwa mshabiki wa chama iwe CCM, CHADEMA, au chama chochote unakuwa mtumwa wa vyama hivyo. Lazima uwe mnafiki. Huwezi kukosoa mapungufu ya chama chako kwa kuhofia kutopewa cheo
 
Kaka Pascal alitegemea hisani kwenye uchaguzi huu. Huoni aligombea?

Ukishakuwa mshabiki wa chama iwe CCM, CHADEMA, au chama chochote unakuwa mtumwa wa vyama hivyo. Lazima uwe mnafiki. Huwezi kukosoa mapungufu ya chama chako kwa kuhofia kutopewa cheo
Kweli kbsaa
 
C😀😀😀😀
 
Ahsante Robert, uandishi wa hali ya juuuuuuu, Great Thinker,
 
Mbeya wamempa Tundu Lissu heshima.

Kwenye video hii hapa chini kuna comments 323 zote zinanena mema kuhusu Tundu Lissu:

 
CCM inawateja wake wa kwenye nyumba za tembe(Simiyu, Singida, Dodoma, Pwani, Tabora, Shinyanga, Geita, Kigoma, Rukwa, Katavi, Lindi, Mtwara, Ruvuma, Songwe na Njombe).
 

Bandiko lako lina ubora wa 80%+. Hii ndio aina ya uchambuzi, sio yale mabandiko ya kina Paskali ya kujiita wazalendo na kujifanya hawaegemei popote. Tena huko kujiita wazalendo wanaanza kwenye paragraph ya mwanzo, badala ya kutuacha tupime wenyewe. Huu ndio uandishi wa kizalendo, na sio huu uzalendo academia wa kina Paskali kuvutia watawala kwa maslahi binafsi.

Cc: Paskali Mayalla
 
Utaanzaje kuingia geti la Ikulu bila ukaribisho wa mwenye kukalia Ikulu?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…