Uchaguzi 2020 Mbeya na Iringa bado ngoma ngumu kwa CCM

Tatizo kubwa la CCM ni kujipa matumaini hewa / Baada ya kuwazuia wapinzani wao wasifungue midomo kwa miaka 5 na baada ya zoezi la hama hama toka Upinzani kuja CCM kwa mwamvuli wa kusaporti juhudi hewa - basi waliona uchaguzi huu bunge litakuwa na 99% CCM.

Baadhi ya watu wengi nikiwemo na mimi nilijua sasa upinzani kwa kheri na tunarudi chama kimoja.

Sasa ndani ya siku si zaidi ya 15 upepo umebadilika kabisa - kwa kweli CCM wasifikiri tena uchaguzi huu ni mwepesi na yawezekana ukawa mgumu kuliko chaguzi zote toka vyama vingi kuasisiwa.
 
Tangu 1995 hadi 2015, watu walichambua, walitabiri, na wengine kudiriki kusema wameoteshwa na Mungu kuwa CCM itaondoka badala yake ndiyo inazidi kujiimarisha zaidi. Namkumbuka hadi TB Joshua alitinga kwa EL kumletea habari ya matumaini-kwamba atashinda na kuchukua nchi. Leo hii mzee wa watu anachunga ng'ombe zake kwa utulivu.

Tufanyeni kazi ili tujipatie kipato, CCM ni nguli wa siasa za Afrika, ni zaidi ya chama cha siasa.

Muulize Lyatonga, Maalim Seif, Dr. Slaha na Edward L watawaelezeni ugumu ulivyo. Maalim amejaribu mara ngapi tena kwa nchi yenye pop less than 500000 iweje uamini kuwa TL atashinda just first attempt kwa nchi yenye wapigakura 29m?

Mi napita tu.....
 
Utapitaje getini bila kibali? Kusema uongo ni dhambi. Au unafikiri Ikulu ni uwanja wa wazi? Hata nyumbani kwako sidhani kuwa naweza kuja tu hivi bila kukaribishwa japo hakuna fensi na geti lenye kuloindwa na FFU.
Sio kila anayeenda Ikulu amekaribishwa mkuu.
Wengine wanaenda kwa mambo yao
 
Tupe list ya iYo mifisafi tafadhali
 
Huu uzi hauendani kabisa na uhalisia uliopohuku mtaani,unge toa uzi huu kabla lisu haja ungesema majimbo yoteccm itachukuwa au chadema imekufa.ushabiki unao uona ni kidogo mno kulinganisha na uhalisia.watu wanao muunga mkono mzee wana free platform ya kuongea sifa zao,wanaokosoa hawana platform ya kuongea maana wametishwa hivyo wanaka nayo moyo.
Kuja kwa lisu kumefanya watu kujitokeza na kuamsha ushabiki kwa wale wasiokuwa na cha kupoteza lakini wafanyabiashara,watu wenye umri,wafanyakazi na wengine bado hawawezi kukosoa wanakaa na machungu yap moyoni watakajitokeza kwenye sanduku la kura
 
Robert, aksante kwa uchambuzi. Ila bado mapema mno kutoa mwelekeo wa jumla. Fanya tafiti zako wiki mbili kabla ya mwisho wa kampeni. Unaweza ukaja na hitimisho sawa na hili au vinginevyo kabisa. "Political results are difficult to predict". We thought, before Lissu came into limelight, opposition in TZ was no more existing. But now the atmosphere is rapidly changing even before formal campaigns begin. Robert, keep your ears on the ground and fingers crossed.
 
Mkuu umeongea mambo makubwa sn. Yaani Ushauri uluoutoa ni mzito sn. Tundu Lissu watu wanakutakia mema sn hadi wanatumia muda wao mwingi kukushauri hata cha kusema na nini cha kufanya. Chadema na Team yenu nzima ya Kampeni, Chukueni haya. Hivi ndio vitu watu wanataka kusikia majukwaani. Mmetafuniwa kila kitu hapo.

..Ila Mkuu Heriel, ningekushauri huu uzi wako ungezitenga kuwa uzi 2. Moja iwe kuhusu Hayo majimbo na nyingine ijitegemee kuhusu Hiyo mipango mkakati na Mambo Muhimu ya Lissu kufanya Ili kushinda Uchaguzi. Uedit, kata kipande cha chini hiki kijitegemee na uandike kichwa chenye kuvuta attention.
 
Mambo ambayo Lisu lazima ayaongelee ili apewe kura na kumzidi Magufuli

Kampeni kampeni bado haijaanza, ni wakati wa kusalimia na kutafuta wadhamini 200 waTanzania wenye kitambulisho cha mpiga kura, usifadhaike kwa Tundu Lissu akizunguka kutafuta wadhamini na kutosikia akinadi sera muda bado.

ila umejaribu kuelezea kero za waTanzania ambazo zitafafanuliwa na kupewa mkakati wa jinsi upinzani utakavyotatau kero hizo.
 
Chadema wakiungana na ACT watapata viti vya ubunge 60 percent na Urais Lissu anashinnda kwa 70 percent ili halina mjadala.
Waungane wasiungane hawawwzi kufikisha kura zaidi ya laki tano

Onyo baada ya tarehe 28/10/2020 hatutaki kusikia habari za kuobiwa kura sawa?
 
Sio Mbeya na Iringa tu. Ni Tanzania nzima CCM imechokwa. Karata yao ni wizi wa kura tu.
Mkuu jisemeee nafis yako kwa taarifa yako CCM itashinda zaidi ya 90 ya viti vya ubunge na udiwani, kama hutaki kula malimao.
 
Uko vizuri Robert Heriel. Digrii yako si ya kuungaunga! Chukua Faru John moja hapo grocery ntakuja kulipa!
 
Tanzania wapiga kura wengi sana ni wanawake hasa wa mama wa nyumbani na wanaume wazee. Vijana ni hovyo kabisa. Ccm tuna mtaji wa kutosha sana.
Mama ntilie, bodaboda na machinga pigeni kura zenu vizuri. Mtajuta, shauri zenu.
 
Ongezea na mifuko ya hifadhi ya jamii, wanachama kuzuiliwa kuchukua mafao hadi afikishe MIAKA 55 how comes mwanachama ambaye ni mwajiriwa wa sekta binafsi ambaye ajira yake ni ya muda mfupi unamwambia asubri MIAKA 55? Hapo magufuli kachemka lissu nayo hiyo ni pointi mhimu kwake
 
Niukweli ulio wazi Lissu hajajipambanua namna ya kusaidia vijana kuhusu ajira hii ni nafasi yake kupata kura,labda kampeni kwakuwa hazijaanza tusubri
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…