Uchaguzi 2020 Mbeya na Iringa bado ngoma ngumu kwa CCM

Usifanye hivyo,
kipimo umpimiacho mtu ndicho utakachopimiwa.

Kwa vile sio kosa kisheria kuwa na tofauti za kimtazamo, usimfanyie hivyo. Kama ameshindwa kukuelewa achana naye
Ah wapi...watu Wana elimu zao lakini mishahara wanayolipywa had unajiskia huruma..wafanyakazi Wana stress Sana kwasasa .sitakiii
 
Holi bandiko wampelekee lissu,akatumie hizi nondo,mwana unazinyaka politiki za bongo kinoma.
 
Kwenye swala la ajira napenda akilizubgumza zitto kabwe, kwani anaeleza kwa fact sana. Maana inatakiwa uelez hizo ajira zinatoka wapi, kama ni serikalini au sector binafsi !
 
Points kama hizi zisizoegemea upande wowote ndo zinatakiwa, mtu akiwa mfuasi wa chama chochote lazima awe mnafiki ambapo itamlazimu kukisifia chama chake tu na kuponda vyama vingine.
 
Mleta mada umejaribu kuelezea ila haujautendea hali uzi wako.
Chadema kwa sasa inakubalika katika mikoa yote, Iringa, Mbeya na Songwe. Chadema vyovyote vile lazima itaongoza kwa kura katika mikoa hii. CCM wakijitahidi mwaka huu watachukua majimbo yasiyozidi 3. Kikubwa zaidi Chadema inakubalika pia sana kwenye mikoa ya Mara, Singida, Manyara, Arusha, Kilimanjaro, Dar es Salaam, Kagera, Pwani na Morogoro. Nimetembea kwenye mikoa hii na nimejionea kwa jinsi gani wananchi walivyo na mwamko mkubwa na Chadema.

Moja ya karata nzuri inakayowaongezea kura nyingi pia Chadema hata kwenye mikoa ya Katavi, Rukwa na Tabora pia ni suala la mgombea wao kuwa Tundu Lissu. Huyu mtu ana bahati sana ya kupendwa na kukubalika. Itoshe kusema there is no way Magufuli ataweza kumshinda Lissu

Kuhusu hoja za Lissu hapo ndo napenda kukukosoa kwa sehemu kubwa.

Hakuna mgombea mwaka huu anayeelezea Sera za Chama chake vizuri kama Tundu Antipas Lissu.

Lissu anaanza kuelezea Sera zake kwa kuanza na matatizo halisi huku akiyaelezea kiufasaha, mwisho ndo anakuja kuelezea sera zake.

Sera za Lissu alizozielezea mpaka sasa zinajibu maswali mengi na hoja nyingi ulizozielezea kwenye uzi wako.

Ni ukweli ulio dhahili kuwa suala la kodi limerudisha nyuma sana uwekezaji Tanzania. Wawekezaji wengi wamefunga ofisi na hata biashara zao ukiacha hawa ambao wamefilisiwa na TRA.
Lissu anaposema anakuja na bill of rights ya walipakodi hapo ni obvious anamaanisha anaenda kutengeneza sekta binafsi imara. Inayokusanya mapato ya uhakika huku iliruhusu biashara na uwekezaji kukua. Hayo yakifanyika lazima ajira zitaongezeka na hali ya uchumi ya wananchi itakuwa nzuri.

Lissu anasisitiza utawala wa haki na sheria. Nadhani hujui, Chadema wamesema ndani ya siku 100 za kwanza watarudisha mchakato wa katiba ya warioba. Labda hujui tu, unapokuwa na katiba nzuri na sheria nzuri huo nao ni moja ya misingi mikuu ya maendeleo kwenye taifa lolote lile. Wawekezaji wa ndani na nje watakuwa na confidence na wewe na hata mifumo ya nchi itafanya kazi vizuri

Mambo mengine mengi Lissu amezidi kuyagusia kwenye kampeni zake na kimapokezi amepokewa vizuri sana.
Naweza pia kusema Lissu ana lugha Nzuri ya kuwasilisha hoja zake. Kwa sasa Naona watu wengi zaidi wakizidi kumpenda zaidi na kumuelewa zaidi kwa namna anavyowapa elimu bora.
 
CCM inawateja wake wa kwenye nyumba za tembe(Simiyu, Singida, Dodoma, Pwani, Tabora, Shinyanga, Geita, Kigoma, Rukwa, Katavi, Lindi, Mtwara, Ruvuma, Songwe na Njombe).
Hapo toa Shinyanga, Geita na kidogo Ruvuma, hao wanajielewa tatizo upinzani huko hawajajipanga, wakikaa vizuri jimbo kama Shinyanga Mjini na Geita mjini ni mali halali kabisa ya Chadema.
 
Mwenzio kafanya uchambuzi, wewe unatuletea siasa za mahaba
 
Wewe huna unachokijua kwenye siasa, umejaa ushabiki tu. Najua baada ya Oktoba utakimbia humu JF
 
naona na namba ya simu umeweka,watakukumbuka mkuu
 
Mwenzio kafanya uchambuzi, wewe unatuletea siasa za mahaba
Huo unaoita uchambuzi katumia chujio gani kuchambua? wewe unaijua nguvu ya Chadema Arusha na Moshi?! au umelishwa zile pumba za Chadema imekufa mpaka umeshiba!.
 
Najua kuwasoma watu, hasa wanafiki lazima atakuwa na mashaka nami
Mkuu ni ngumu sana hasa wakishajua hupendi waipigie kura CCM, watapretend mpaka utaamini tu. Kampeni zikianza rasmi wengi watamuelewa Lisu tu.
 
Mkuu ni ngumu sana hasa wakishajua hupendi waipigie kura CCM, watapretend mpaka utaamini tu. Kampeni zikianza rasmi wengi watamuelewa Lisu tu.
Naamini kabisa huyu ndio mkombozi wa watanzania, sipendi siasa lakini jamaa anasifa za uongozi kwa kiasi kikubwa, kuliko hicho kikundi kingine, tuombe mungu tubadili upepo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…