Lady Whistledown
JF-Expert Member
- Aug 2, 2021
- 1,147
- 2,008
Naibu Waziri wa Afya, Dkt, Godwin Mollel amesema wamebaini kuwa Polyclinic moja imetoweka na Tsh. Millioni 137 za NHIF ambayo waliibaini kutoa huduma kwenye nyumba ya wageni na walipoifuatilia ili kuwakamata wahusika walitoweka kusikojulikana hadi hii leo.
Pia akiwa katika kikao cha Kamati ya Bunge ya Maendeleo ya Jamii hivi karibuni jijini Dar es Salaam, Dk Mollel alisema, wataalamu walioagizwa kufanya uchunguzi wamebaini ubadhilifu wa Tsh. Bilioni 1.6 za NHIF Mbeya mjini pekee.
Hii ni baada ya Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu kuipa NHIF siku 14 za kumpelekea mikakati ya kudhibiti udanganyifu unaofanywa kwa kutumia mifumo ya TEHAMA na wateja wake.
Chanzo: Mwananchi