JanguKamaJangu
JF-Expert Member
- Feb 7, 2022
- 2,780
- 6,607
Mnamo tarehe 26.03.2022 majira ya saa 13:30 mchana, Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya lilifanya msako huko kijiji cha Nsongwi Mantanji, Kata ya Ijombe, Tarafa ya Tembela, Wilaya na Mkoa wa Mbeya na kufanikiwa kumkamata FIDELIS KOMBA [42] Mganga wa tiba asilia, Mkazi wa Nsongwi – Mantanji akiwa na noti 219 za Tshs 10,000/= zote zikiwa na namba KL 4105891 na noti 230 za Tshs.5,000/= zote zikiwa na namba HF 4424893 zinazodhaniwa kuwa ni noti za bandia.
Mtuhumiwa kabla ya kukamatwa alitajwa na mtuhumiwa mwenzake aitwaye FERUZ SELEMAN [35] Fundi ujenzi na Mkazi wa majengo mapya Nsalaga ambaye alikamatwa tarehe 25.03.2022 majira ya saa 20:45 usiku huko maeneo ya Isyesye -Madukani, Kata ya Isyesye, Tarafa ya Iyunga, Jijini Mbeya akiwa na noti bandia 69 za Tshs 5,000 zote zikiwa na namba HF 4424893.
Hivyo, kufanya jumla ya noti 299 za Tshs.5,000/= akiwa katika harakati za kutaka kuziingiza kwa wakala wa mitandao ya fedha kwa nia ya kuzihalalisha fedha hizo na baada ya kuhojiwa kwa kina ndipo alimtaja FIDELIS KOMBA kuwa ndio aliyempa noti hizo. Upelelezi wa shauri hili unaendelea ili kubaini mtandao mzima wa watu wanaojihusisha na utengenezaji na usambazaji wa noti bandia.
Imetolewa na:
[ULRICH O. MATEI – SACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.