Erythrocyte
JF-Expert Member
- Nov 6, 2012
- 128,308
- 245,426
Akizungumza kwenye Mkutano wa Hadhara kwenye Kata ya Iyunga, Joseph Mbilinyi ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kanda ya Nyasa, amewatahadharisha wazazi kuchunga watoto wao ambao hawakutimiza miaka 18 ili wasiingie matatizoni kwa kutumika kujiandikisha kwenye uchaguzi wa serikali za Mitaa, Kitakachowapata wasije wakamlilia mtu
Ikumbukwe kwamba Chadema Kanda ya Nyasa imeweka CALL CENTER kwa ajili Wananchi kuwasilisha hujuma zote zinazohusu Uandikishaji wa wapiga kura
Tayari jambo hili muhimu limeanza kuleta tija baada hujuma kibao kuripotiwa na kufichuliwa.
Itakumbukwa Rais Samia jana aliwakumbusha Wananchi kwamba Uchaguzi wa Serikali za Mitaa usichukuliwe Poa, na ndivyo Kanda ya Nyasa inavyofanya.