LGE2024 Mbeya: Sugu atahadharisha Wazazi kuhakikisha Watoto wao wa under 18 wasijiandikishe ili kutumika kwenye Uchaguzi, kitakachowapata wasimlilie Mtu

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024

Erythrocyte

JF-Expert Member
Joined
Nov 6, 2012
Posts
128,308
Reaction score
245,426


Akizungumza kwenye Mkutano wa Hadhara kwenye Kata ya Iyunga, Joseph Mbilinyi ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kanda ya Nyasa, amewatahadharisha wazazi kuchunga watoto wao ambao hawakutimiza miaka 18 ili wasiingie matatizoni kwa kutumika kujiandikisha kwenye uchaguzi wa serikali za Mitaa, Kitakachowapata wasije wakamlilia mtu



Ikumbukwe kwamba Chadema Kanda ya Nyasa imeweka CALL CENTER kwa ajili Wananchi kuwasilisha hujuma zote zinazohusu Uandikishaji wa wapiga kura



Tayari jambo hili muhimu limeanza kuleta tija baada hujuma kibao kuripotiwa na kufichuliwa.

Itakumbukwa Rais Samia jana aliwakumbusha Wananchi kwamba Uchaguzi wa Serikali za Mitaa usichukuliwe Poa, na ndivyo Kanda ya Nyasa inavyofanya.
 
Leo ndo nimeshtuka sasa ebwana huu uandikishaji ulishafanyika tangu August. Iko hivi mwezi August mtaani kwetu walipita watu wa CCM wakiongozwa na mwenyekiti eti walikua wanaandika majina ya wakazi wote wa mtaa ule😁😁...sasa nilivyosikia uchaguzi serikali za mitaa wanaandikisha majina tu ndo nikapata picha kua hawa jamaa wana mbinu kinoma za kuiba.
 
Tutawadhibiti vibaya mno!
 

Si itakuja mijitu mizima kutumia majina hayo siku ya kupiga kura?
 
Si Mbeya tu, vyanzo vyangu vinaniambia ni mikoa karibu yote.

Yaani wanafunzi wanafundishwa wizi wa kura wakiwa WADOGO.

Wakiwa na family zao, Maadili watayatoa wapi kuwafundisha watoto wao!
 
Dawa ni kuakikisha kila mtaa ,kitongoji nchi zima wapinzani wanasimamisha wagombea , na kila mgombea kuakikisha anao mawakala makini katika vituo vyake eneo husika ,tuone kura za kwenye vyumba vyao walizopiga kwa watu feki watazipitisha wapi ,

Katika hili ccm hawana washauri pamoja na yote watapigwa kama ngoma tu, kama wapinzani watajipanga vizuri
 
Si Mbeya tu, vyanzo vyangu vinaniambia ni mikoa karibu yote.

Yaani wanafunzi wanafundishwa wizi wa kura wakiwa WADOGO.

Wakiwa na family zao, Maadili watayatoa wapi kuwafundisha watoto wao!
Wasimlilie mtu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…