KERO Mbeya: TARURA sambazeni vifusi mlivyomwaga tangu Mwaka 2024 katika Barabara ya Sangu kwenda Benki Kuu

KERO Mbeya: TARURA sambazeni vifusi mlivyomwaga tangu Mwaka 2024 katika Barabara ya Sangu kwenda Benki Kuu

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua

Mwanongwa

JF-Expert Member
Joined
Feb 15, 2023
Posts
611
Reaction score
567
Hivi TARURA Mkoa wa Mbeya, kilichowafanya mkamwaga vifusi kwenye hii Barabara ya kutokea Shule ya Sekondari Sangu kuelekea Benki Kuu na kuviacha bila kusambaza ni nani?

Barabara ni mbovu mlivyoanza kumwaga vifusi tukajua mmekuja kututatulia tatizo lakini badala yake mmeongeza tatizo juu ya tatizo. Sambazeni hivyo vifusi bhana, haiwezekani tangu Mwaka jana (2024) vifusi mpaka leo vipo tu havijasambazwa.

Hii nayo imekuwa kero kubwa ni bora mngeiacha kama ilivyokuwa hii Barabara kuliko mlivyofanya, mmesababisha barabara imekuwa nyembamba na changamoto kupitika kwa wanaopita na magari.

DSC_0752.JPG
DSC_0755.JPG
DSC_0742.JPG
DSC_0740.JPG


Pia soma:
~
Hatimaye Vifusi vya Barabara ya Sangu (Mbeya) kuelekea Benki Kuu vilivyokuwa kero, vimesambazwa

~ Mbeya: Chemba ya Maji taka Mitaa ya Forest ya Zamani inamwaga maji ya kinyesi mtaani na inachukulia poa tu
 
MKuu itv juzi wamesema mkandarasi awajalipwa helà zaoo mvumiliane Tena n huko mbeya
 
Hatari sana

I
HATAREEE NA SIDHAN KAMA WAKUU WANAJUA..KUNA NJIA MOJA JAMAA ALIGOMA KUENDELEA NIKAIWASHA. HUMU MAKANDARASI WALIPWE. JAMAN KAZI HAMNA TAURA WEWEE MWEZI JAMA WAKO KAZINI..SASA HII YA MBEYA OFISI YENYEWE WALITANGAZA KAZI IPOO
 
Back
Top Bottom