Waandishi Wasaidizi na Waendesha vifaa vya Bayometriki wa Kata 33 za Wilaya ya Kyela, Mkoa wa Mbeya wakila kiapo kabla ya kuanza mafunzo ya siku mbili leo tarehe 23 Disemba, 2024.
Mafunzo hayo ni sehemu ya maandalizi ya zoezi la uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura unaotarajiwa kufanyika katika mikoa ya Mbeya, Iringa na Dodoma katika Halmashauri ya wilaya ya Mpwapwa kuanzia tarehe 27 Desemba, 2024 hadi tarehe 02 Januari, 2024.
Vituo vya kuandikisha wapiga kura vitafunguliwa kuanzia saa 2:00 asubuhi na kufungwa saa 12:00 jio