Mbeya: Wafanyabiashara Mbalizi na Uyole wapewa Elimu ya Kodi

Mbeya: Wafanyabiashara Mbalizi na Uyole wapewa Elimu ya Kodi

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
3,984
Reaction score
13,760
Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imeanza kutoa elimu ya Kodi kwa wafanyabiashara wa mkoa wa Mbeya katika kampeni maalumu ya Elimu ya Kodi mkoa kwa mkoa.

Kampeni hiyo iliyoanza tangu Machi 9, inaendelea hadi Machi 14, 2020 ambapo wafanyabiashara wa eneo la Mbalizi na Uyole wamepewa elimu ya utunzaji wa kumbukumbu za biashara ili waweze kulipa Kodi sahihi na kwa wakati.

Akizungumza wakati wa zoezi hilo, Afisa Huduma na Elimu kwa mlipakodi wa mkoa wa Mbeya, Serapio Luanda amesema TRA inalenga kutoa elimu ya Kodi kwa wafanyabiashara na wananchi wa mkoa wa Mbeya ili kila mfanyabiashara atambue haki na wajibu wake katika kulipa kodi ikiwa ni pamoja na wajibu wa TRA kama mkusanyaji Kodi za serikali.

Aidha, amewataka wafanyabiashara kutunza kumbukumbu za biashara kwani ndicho kigezo kikubwa kinachotumika wakati wa ukokotoaji wa Kodi ambayo mfanyabiashara anastahili kulipa kwa mujibu wa sheria za Kodi.

"Tunafanya kampeni ya Elimu ya Kodi kwa wafanyabiashara na wananchi ili wafahamu sheria za Kodi na utaratibu unaotumiwa na TRA katika ukusanyaji wa Kodi" amesema Luanda.

Amesema TRA inafanya kampeni ya elimu ya Kodi mkoa kwa mkoa ikilenga kuwaelimisha wafanyabiashara na wananchi kwa ujumla masuala mbalimbali yanayohusu ulipaji kodi ikiwemo haki na wajibu wa Mlipakodi, umuhimu wa utunzaji wa kumbukumbu za biashara, madhara ya biashara za magendo mipakani pamoja na njia za kielektroniki za ulipaji kodi ya majengo na Kodi za mapato kwa wakati.

Ameongeza kuwa katika mkoa wa Mbeya kampeni ya elimu kwa Mlipakodi itafanyika katika Wilaya za Mbeya mjini, Kyela, Chunya na Mbarali.
IMG-20200310-WA0037.jpg

Afisa Huduma na Elimu kutoka TRA, Julieth Kidemi akimwelekeza mfanyabiashara wa Uyole namna ya kutunza kumbukumbu za biashara wakati wa kampeni ya elimu kwa Mlipakodi inayoendelea mkoani Mbeya.
 
Back
Top Bottom