Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 3,984
- 13,760
Mahakama ya Wilaya Kyela Mkoani Mbeya, Septemba 1, 2022 ilitoa hukumu ya mashauri mawili.
Kwanza ni Shauri ya Jinai Na.91/2021 (R v Never Black Mwakalinga na Holdin Jaji), ambapo mshtakiwa wa kwanza Bi. Never Black Mwakalinga alikuwa Wakala wa Pembejeo za Kilimo katika Kijiji cha Mwaya na mshtakiwa wa pili Holdin alikuwa Afisa Mtendaji wa Kijiji cha Mwaya ambao kwa pamoja walikuwa wakishtakiwa kwa makosa ya kughushi vocha za pembejeo za kilimo.
Watuhumiwa hao walisaini sehemu ya wakulima wanufaika wa pembejeo za kilimo za ruzuku kuonesha kuwa wakulima husika wamepokea pembejeo huku wakijua kuwa ni uongo.
Kwenye uamuzi wake Mahakama iliwatia hatiani kwa makosa yote na kuamriwa kila mmoja kwenda jela miaka mitatu.
Shauri la pili, la Jinai Na. 92/2021 Jamhuri dhidi ya Bahati Nelson na wenzake wawili, ambapo mshtakiwa wa kwanza Bahati alikuwa Afisa Mtendaji katika Kijiji cha Lukuyu, mshtakiwa wa pili Bi. Never Black Mwakalinga alikuwa Wakala wa kusambaza pembejeo katika Kijiji cha Lukuyu na mshtakiwa wa tatu Justin Jaji alikuwa Mwenyekiti wa Kamati ya pembejeo katika Kijiji cha Lukuyu.
Wote kwa pamoja walikuwa wanashtakiwa kwa makosa ya kughushi Vocha za pembejeo za kilimo zenye ruzuku.
Kwenye uamuzi wake Mahakama iliwatia hatiani washtakiwa wote watatu kwa makosa ya kughushi na kuwapa adhabu za kila mmoja kwa makosa aliyotiwa hatiani kwenda jela miaka miwili.