Mbeya waonywa kugeuza pombe dawa ya Corona

Mbeya waonywa kugeuza pombe dawa ya Corona

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2012
Posts
5,108
Reaction score
10,191
Wakazi mkoani Mbeya wametakiwa kuepuka matumizi ya vilevi vikali kwa kuamini ni dawa inayoweza kupambana na homa ya mapafu inayosababishwa na virusi vya corona.

Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Albert Chalamila (pichani) alitoa onyo hilo jana alipozungumza na waandishi wa habari juu ya jitihada mbalimbali zinazofanywa na wadau mkoani hapa katika kukabili maambukizi ya virusi vya corona.

Alisema wapo watu wanaoamini wanaweza kutumia pombe kali kujipaka au kunywa wakiamini ni kinga dhidi ya virusi vya corona. RC Chalamila alisema habari hizo si za kweli na hazipaswi kuaminiwa na watu na hatua hiyo inaweza kuleta madhara zaidi kwa maambukizi.

“Ni kweli wanasema vitakasa mikono vinatajwa kuwa na kilevi cha hali ya juu. Hii isiwafanye watu wa Mbeya kununua K Vant au konyagi na kujipaka wakiamini wanajilinda,”alisisitiza.

Alisema kuna baadhi ya watu mkoani hapa wanaielezea corona kwa vitisho vikubwa na pia upotoshaji kuaminisha wenzao ukipimwa muda huo huo na majibu yake yanapatikana haraka.

Akizungumzia mkoa ulivyojipanga mapambano ya virusi vya corona, alisema tayari kila wilaya imetenga vituo maalumu vya afya kutoa huduma itakapotokea kuwepo kwa wagonjwa au watu wanaohisiwa kuwa na maambukizi hayo.

Alisema ushirikiano kati ya Mkoa wa Mbeya na mikoa jirani ikiwemo Songwe unaendelea kuhakikisha utaratibu wa kufuatilia kwa karibu watu wanaoingia kwa ndege, treni na mabasi

Habari Leo
 
Back
Top Bottom