Decree Holder
JF-Expert Member
- Jul 19, 2015
- 2,559
- 3,745
Kuruthum Omary Kahimba & Rehema Omary Kahimba
vs
Mwajuma Omary Kahimba, Misc Civil Cause No 04 Of 2018
Kwa maneno yake mwenyewe Jaji Ndunguru anasema kesi hii inamkumbusha mistari ya Biblia Takatifu kutoka kitabu Cha Yohana Mtakatifu 14;8. Yesu alipokuwa akifundisha mmoja wa wanafunzi wake "Filipo akamwambia, Bwana, utuonyeshe Baba, yatutosha. Yesu akamwambia, mimi nimekuwepo pamoja nanyi siku hizi zote, wewe usinijue, Filipo? Aliyeniona mimi amemwona Baba; Basi wewe wasemaje, utuonyeshe Baba? Husadiki ya kwamba mimi ni ndani ya Baba na Baba Yu ndani yangu?
Katika kesi hii Rehema na Kuruthum walimburuta mama yao mzazi mahakamani wakiomba mahakama imuamuru/imlazimishe mama yao mzazi awatajie na kuwaonyesha baba yao mzazi (biological father) na baadaye akishakufanya hivyo mahakama imuamuru/imlazimishe baba yao wakapime DNA. Waombaji waliieleza mahakama kuwa wamejaribu kumuomba mama yao awatajie jina na kuwaonyesha baba yao mzazi bila mafanikio. Wamejaribu njia zote za amani ikiwemo kupitia vikao vya ukoo lakini mama yao mzazi amekataa kuwatajia na kuwaonyesha baba yao badala yake amekuwa akiwaambia kuwa wao ni "zawadi kutoka Kwa Mungu" na kwamba yeye hafahamu baba yao mzazi alipo. Ilielezwa mahakamani kwamba Kuruthum na Rehema walilelewa na Babu yao mzaa mama baada ya mama yao kuolewa na mwanaume mwingine. Wanadai wamekosa si tu upendo wa baba Bali hata upendo wa mama na Sasa Mama yao anawanyima haki yao ya msingi ya kumfahamu Baba yao mzazi (biological father)
Ni kesi iliyoshughulisha Mahakama kuu, Mbeya. Mahakama inasema maswali ni mengi kuliko majibu; Je mahakama inayo mamlaka ya kumlazimisha mjibu maombi (Mama mzazi) kuwatajia na kuwaonyesha waombaji baba yao? Kama jibu ni ndiyo chini ya sheria gani? Na ni kwanini mama yao anakataa kuwatajia na kuwaonyesha baba yao mzazi? Je waombaji wana nafuu au njia nyingine yoyote wanayoweza kuitumia kujua baba yao ni nani? Kama mahakama ikitoa amri inayoombwa itatekelezeka? Na kama akiwatajia na kuwaonyesha baba yao mzazi mahakama inaweza kumlazimisha kupima DNA ikiwa yeye siyo sehemu ya kesi hii?
UAMUZI WA MAHAKAMA
1. Watoto wadogo kisheria Wana haki ya kushitaki kujua baba yao ni nani Ili wapate huduma za msingi kutoka Kwa baba yao. Na pia Kwa sababu za kiafya kama (Genetics and medical history) pale inapobidi. Hata hivyo waombaji siyo watoto wadogo walio chini ya miaka 18, umri wao ni kati ya miaka 40 na 50. Walilelewa na Babu mzaa mama na walipewa mahitaji yote ya msingi kama watoto wengine.
2. Amri zinazoombwa mahakamani hazitekelezi.
Mama yao ameshasema hafahamu baba yao mzazi alipo na sababu zinaweza kuwa nyingi sana kama ifuatavyo.
i) Watoto walipatikana Kwa kubakwa na mama angependa hilo libakie kuwa Siri
ii)Wakati wa mimba kutungwa mama alijihusisha kimapenzi na wanaume wengi hivyo hajui ni nani aliyempa mimba
iii) Mama hakumbuki na wala hafahamu ni nani alifanya naye mapenzi mpaka kupelekea mimba.
iv) Mama alipata mbegu kutoka Kwa wachangia mbegu (Sperm Donor) hivyo angependa kutunza privacy ya anonymous sperm donor. Au hata hana access ya taarifa za huyo anonymous sperm donor.
3. Hata kama akitajwa mahakama haiwezi kumlazimisha baba mzazi kupima DNA kwani siyo sehemu ya kesi (stranger)
Mahakama inasema ni vyema kuweka mizania sawa kati ya haki ya watoto kumjua baba yao mzazi (biological father) na haki ya faragha ya mama yao mzazi, ikizingatia kuwa mama yao alijitoa kuhakikisha wanapata haki zote za msingi kama watoto wengine. Jaji anasema kuamua vinginevyo kutasababisha mafuriko ya kesi za aina hii ambapo watoto watashitaki mama zao kudai waambiwe nani baba zao.
Mahakama ikaenda mbali kushauri watoto kutafuta njia nyingine za kujua ukweli kuhusu baba yao mzazi kama vile kutangaza kwenye magazeti na luninga kuliko kutonesha vidonda vya mama yao.
Mahakama ilitupilia mbali maombi ya watoto kutaka mahakama imlazimishe mama yao mzazi awatajie na kuwaonyesha baba yao mzazi (biological father)
"No one can object that a mother can be mutually a mom and a dad. As hinted above, when gave an example when Philip asked Jesus to reveal who is the Father, Jesus was keen enough to declare that, since they have seen him, they have inevitably seen the Father. The same applied to this application. Single mothers or all mothers who raised their
children alone, in the absence of their father must be respected and honored. They are everything to their children. The child who received all the required support from his/her mother needs not to awaken the healing wounds of his mother who worked hard day and night to ensure that the child is safe and sound. Even if the court could compel the respondent to name the identity of the applicants' father, the execution of the order could be very difficult....." Ndunguru, J
MY TAKE;
Ukiachana na final verdict ya Mahakama, Mheshimiwa Jaji ametaja sababu nyingi sana za kwanini amri haitekelezeki ambazo hazikutajwa na mjibu maombi (Mama mzazi). Hii imekuwa kama Jaji alikuwa anamlisha maneno mjibu maombi, mama alikuwa mchumi wa maneno na Wala hakufika hatua ya kueleza ni ugumu gani anaoupata kuwatajia na kuwaonesha Baba yao mzazi (biological father) watoto wake.
UNA MAONI GANI?
Wakili Zawadi B. Lupelo
Whatsapp;0755106783