Mwanongwa
JF-Expert Member
- Feb 15, 2023
- 611
- 567
Bwana Erick Lucas Simtengu [24] mkazi wa Kijiji cha Mbugani Wilayani Chunya amehukumiwa kifungo cha miaka 30 jela baada ya kukutwa na hatia ya kumbaka mwanafunzi wa kidato cha pili katika Shule ya Sekondari Isenyela mwenye umri wa miaka 15 [Jina linahifadhiwa].
Hukumu hiyo imetolewa katika Mahakama ya Wilaya ya Chunya mbele ya Hakimu Mheshimiwa.James Mhanus Novemba 12, 2024 na Mwendesha Mashitaka wa Jeshi la Polisi Mkaguzi wa Polisi Kahiwa Mayanja ambapo mshitakiwa alitenda kosa hilo Julai 17, 2024 baada ya kumtorosha mhanga kutoka kwenye Bweni la Shule usiku na kumpeleka nyumbani kwake na kufanya naye mapenzi hadi asubuhi.
Vile vile, Modrick Elias Mwakibete [21] mkazi wa Uyole Jijini Mbeya amehukumiwa kifungo cha miaka 30 jela kwa kosa la kubaka alilolifanya kwa mtu mzima [Jina linahifadhiwa] baada ya kumtishia kumchoma kwa kisu na kisha kutimiza adhima yake.
Hukumu hiyo imetolewa katika Mahakama ya Wilaya ya Kyela mbele ya Hakimu Mheshimiwa Paul Barnabas na Mwendesha Mashitaka wa Polisi Mkaguzi Msaidizi wa Polisi Bihemo Dawa Mayengela ambapo mshitakiwa alitenda kosa hilo Machi 23, 2024 baada ya kuwasiliana na kukutana na mhanga kisha kubadilisha mad ana kumlazimisha wafanye mapenzi huku akimtishia kumchoma kisu ambacho alikuwa nacho.
Hukumu hizo zimetolewa kwa mujibu wa kifungu cha 130 kifungu kidogo cha kwanza na cha pili (b) na kifungu cha 131 kifungu kidogo cha kwanza vyote vya sheria ya kanuni ya adhabu.