Mbeya: Wawili wahukumiwa kunyongwa Hadi kufa baada ya kukutwa na hatia ya mauaji

Mbeya: Wawili wahukumiwa kunyongwa Hadi kufa baada ya kukutwa na hatia ya mauaji

Mwanongwa

JF-Expert Member
Joined
Feb 15, 2023
Posts
611
Reaction score
567
Mahakama Kuu Kanda ya Mbeya imewahukumu kunyongwa hadi kufa Emanuel Patson Mwesya [24] na David Saimon Mwalindu [25] wote wakazi wa Mji wa Tunduma Mkoa wa Songwe baada ya kukutwa na hatia kwa kosa la mauaji walilolifanya kwa kumuua Lufingo Asumwisye [37] aliyekuwa Mkazi wa Kijiji cha Bitimanyanga Wilaya ya Chunya Mkoani Mbeya.

Hukumu imetolewa na Mheshimiwa Jaji wa Mahakama Kuu Kanda ya Mbeya Aisha Pinda na Mwendesha Mashitaka wa Serikali Veneranda Masai Novemba 19, 2024 kwa mujibu wa vifungu namba 196 na 197 vyote vya sheria ya kanuni ya adhabu, washitakiwa walitenda kosa hilo Januari 01, 2022 baada ya kumvizia Lufingo Asumwisye akiwa shambani kwake kisha kumuua kwa kumkata kwa kitu chenye ncha kali kichwani kisha kumuibia Pikipiki yake.

Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linatoa rai kwa baadhi ya wananchi wanaendelea kufanya vitendo vya uhalifu kuacha kwani uhalifu haulipi na badala yake watafute shughuli nyingine za kufanya ili kujipatia kipato halali. Aidha, Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linatoa wito kwa wazazi na walezi kuimarisha ulinzi wa mtoto hasa katika kipindi hiki cha kuelekea sikukuu za mwisho na mwanzo wa mwaka ili kuwaepusha na hatari ikiwemo vitendo vya ukatili na unyanyasaji.

Imetolewa na:
Benjamin Kuzaga – SACP
Kamanda wa Polisi,
Mkoa wa Mbeya

KAIMU RPC.JPG
 
Back
Top Bottom