Mwanongwa
JF-Expert Member
- Feb 15, 2023
- 611
- 567
Naomba leo niwape angalizo kidogo hasa sisi wenye Watoto ambao ni Wanafunzi, tujaribu kuwapa Elimu ya usafi na kujiepusha kula kula hovyo huko mashuleni.
Hali ya Kipindupindu ndani ya Jiji hili ni mbaya sana tena sana, Wagonjwa wamekuwa wakiongezeka kila siku, huku idadi ya vifo pia ikiongezeka.
Kutokana na hali hii hofu imekuwa kubwa huko shuleni ambako watoto wetu wanakwenda kusoma, je kutakuwa salama?
Taarifa nilizonazo ndugu yenu ni kwamba hospitali ya Igawilo imezidiwa na Wagonjwa wa kipindupindu, hivyo wameongeza Vituo vya kuwahudumia Wagonjwa wa kipindupindu ambavyo ni Iganzo na Ndanyela kilichopo Kata ya Iyunga.
Kitendo cha Kuongezea Vituo, hivyo ni ishara tosha kuwa kipindupindu kimetamalaki ndani ya Jiji la Mbeya.
Sasa nawaibia siri ninyi wenye mamlaka piteni ndani ya Soko la Sido Kuna migahawa ni michafu balaa.
Mwanongwa nawakumbusha tu ndugu zangu tuzingatie sana usafi katika maeneo yetu yanayotuzunguka ili kupambana na ugonjwa huu.
Serikali nayo imekuwa ikitoa taarifa kwa kusuasua kuhusu mwendeleo wa hali ya Ugonjwa wa Kipindipindu Mkoani hapa, sijui kwanini wanashindwa kuwa na uwazi ili watu wajue uhalisia na wajue hatua za kuchukua.
Pia soma:
~ Wagonjwa wa Kipindupindu wafikia 22 Mbeya, na Serikali imepiga kimya!
~ Utaratibu wa uzoaji Taka Jiji la Mbeya ni shida, zimezagaa mitaani licha ya Wananchi kulipa ili zizolewe